Na Mwandishi Wetu , TimesMajira Online, Morogoro
WAJUMBE wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), wamepiga kura ya kuchagua wajumbe saba wa Kamati ya Utendaji ya jukwaa hilo, katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo mkoani Morogoro.
Wajumbe hao wataungana na washindi wa nafasi ya Mwenyekiti, Deodatus Balile na Makamu Mwenyekiti, Bakari Machumu,, walioshinda katika uchaguzi huo na kutangazwa na Kamati ya Uchaguzi ili kuliendesha jukwaa hilo katika kipindi cha miaka minne.
Walioshinda ni Salim Said Salim, Yassin Sadick, Simon Mkina, Neville Meena, Jane Mihanji na Lilian Timbuka.
Wagombea katika bodi hiyo walikuwa 11 ambao ni Nevile Meena (62 ), Taus Caren Mbowe (45), Jane Mihanji (63), Lilian Timbuka ( 55), Sadik Yassin (69).
Wengine ni Angel Akilimali ( 48), Simon Mkina (69),Salim Salim Kura (75 )
Hata hivyo wagombea Saed Kubenea na Joyce Shebe walijitoa katika kinyang’anyiro hicho. Hivyo wagombea saba ndio walipitishwa kuwa wajumbe wa bodi ya TEF.
More Stories
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu