Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 5, 2020 amekamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi wa leo, Rais Magufuli amewateua Mawaziri 21 ambao wataungana na Mawaziri wawili walioteuliwa Novemba 13, 2020, na amewateua Naibu Mawaziri 23. Aidha,Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wabunge wawili ambao pia amewateua kuwa Mawaziri.
Pia,Rais Magufuli ameongeza wizara mpya moja ambayo ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Mawaziri walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mhandisi Elias John Kwandikwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Kept. Mst. George Huruma Mkuchika kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. William Vangimembe Lukuvi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Jumaa Hamidu Aweso kuwa Waziri wa Maji.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Jenister Joakim Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) aliyekuwa akishughulikia Afya, pia ameteuliwa na Mhe. Rais Magufuli kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji)
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Selemani Saidi Jafo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Medard Matogolo Kalemani kuwa Waziri wa Nishati.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Leonard Chamuriho kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.
Mhandisi Chamuriho ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi, pia ameteuliwa na Mhe. Rais Magufuli kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Adolf Faustine Mkenda kuwa Waziri wa Kilimo.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa Waziri wa Madini.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. George Boniface Taguluvala Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Ummy Ally Mwalimu kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Hata hivyo, tayari Rais Magufuli alishawateua na kuwaapisha mawaziri wawili ambao ni Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye ni Waziri wa Fedha na Mipango na Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Naibu Mawaziri walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Kigahe Exaud Silaoneka kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Angelina Sylvester Lubala Mabula kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Patrobas Paschal Katambi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Khamis Hamza Khamis kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mwanaidi Ali Khamis kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Kipanga Juma Omary kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Festo Stephen Dugange kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Byabato Stephen Lujwahuka kuwa Naibu Waziri wa Nishati.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. John Deogratius Ndejembi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Pauline Philipo Gekul kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Ndulane Francis Kumba kuwa Naibu Waziri wa Madini.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Msongwe Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Ummy Hamis Nderinanga kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mhandisi Marryprisca Winfred Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Maji.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Abdallah Hamis Ulega kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. William Tate Ole Nasha kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Marry Francis Masanja kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. David Ernest Silinde kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Hussein Mohamed Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Godwin Oloyce Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Geophrey Mizengo Pinda kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.
Aidha, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa wateule wote wataapishwa wiki ijayo jijini Dodoma kwa tarehe na muda utakaotangazwa baadaye.
More Stories
Rais Samia afanya uteuzi
TARURA Kilimanjaro yatimiza ahadi ya Rais Samia
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria