
Na Moses Ng’wat, Mbozi
MKUU wa Mkoa wa Songwe, Abubakri Kunenge, amesema hajafika mkoani humo na miujiza, bali anahitaji ushirikiano wa wadau na wananchi ili kuharakisha maendeleo.
Amesema mafanikio ya Songwe hayawezi kupatikana kwa Serikali pekee, akiwataka viongozi, watendaji, sekta binafsi na wananchi kufanya kazi kwa pamoja kuongeza uzalishaji na kuchochea shughuli za kiuchumi.
Kunenge ametoa kauli hiyo, Septemba 23, 2026, wakati wa kikao na wadau wa sekta binafsi katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Selewa, Wilaya ya Mbozi.

Kikao hicho kilikuwa kwa ajili ya kujitambulisha kwa wadau hao wa sekta, ikiwemo kujadili mafanikio, fursa na changamoto za biashara na uwekezaji, pamoja na namna ya kuweka mikakati ya kuboresha mazingira ya kufanya shughuli hizo mkoani humo.
“Ngoja niwaambie, nimekuja hapa sina miujiza, kikubwa naombeni ushirikiano ili kuharakisha maendeleo…na mimi naamini hatuwezi kushindwa,” amesema Kunenge.
Amesema ushirikiano huo unapaswa kuelekezwa pia katika kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa Songwe, kuongeza uzalishaji na kutumia fursa zilizopo kuchochea uchumi wa mkoa.

Aidha, Kunenge amesisitiza matumizi ya takwimu katika kupima matokeo ya mipango ya maendeleo, huku akiwaonya watendaji na wataalamu wa Serikali dhidi ya ukilitimba unaoweza kuchelewesha utekelezaji wa mipango hiyo ya maendeleo mkoani humo.
Amesema kila kiongozi, mtendaji na mwananchi ana wajibu katika maendeleo ya Songwe, hivyo hakuna anayepaswa kufanya kazi kwa maslahi yake binafsi badala yake atangulize malengo ya Mkoa.
Kunenge ameanza kutekelez majukumu yake kwa kuita makundi mbalimbali wa maendeleo kwa lengo la kujitambulisha.


More Stories
Watanzania waonywa matumizi holela ya dawa
Madereva guta 72 wakamatwa,waonywa kuhusu usalama
Mweli:Wazee ni muhimu kwa maendeleo