Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Wizara ya Nishati inaendelea kuhakikisha elimu kuhusu nishati safi ya kupikia inawafikia wananchi wa makundi mbalimbali ikiwemo kuanzia ngazi ya elimu ya awali, ili watoto wakue wakifahamu maana ya nishati safi ya kupikia, faida zake pamoja na madhara ya kutumia nishati zisizo safi.
Elimu hiyo leo imewafikia wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Lucia kutoka Wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya NaneNane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.

Wanafunzi hao wameelezwa kuhusu aina mbalimbali za nishati safi ya kupikia na umuhimu wake katika kulinda afya, mazingira na kuokoa muda.



More Stories
JKT kutoa elimu hata baada ya Nanenane
Ndejembi:Afrika itumie gesi asilia kuharakisha upatikanaji wa Nishati Safi ya Kupikia
Serikali yaagiza usalama migodini Lindi