July 26, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Miundombinu ya shule yatakiwa kulindwa

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online- Mbeya

UONGOZI wa shule ya msingi Iwindi iliopo mkoani Mbeya pamoja na wananchi,wametakiwa kuhakikisha miundombinu ya shule hiyo inalindwa ili idumu na kuendelea kutoa huduma bora za elimu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Beno Malisa, alizungumza hayo jana,alipofanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi kuhusu utoaji wa huduma za kijamii na uwajibikaji wa Serikali.

Akiwa katika shule ya msingi Iwindi,Malisa alikagua miundombinu mbalimbali iliyojengwa kwa fedha za Serikali ikiwemo vyumba vya madarasa, ofisi za walimu na matundu ya vyoo,ambapo amesema,ameridhishwa na ubora wa utekelezaji wa mradi huo.

“Mradi huu umetekelezwa vizuri,sasa ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha miundombinu hii inalindwa kwa kuwa ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwa manufaa ya jamii,”amesema Malisa.

Pia amesema,kila mwananchi akawe balozi wa kuitunza ili iendelee kuwahudumia watoto wao kwa muda mrefu.

Akisoma taarifa ya utekekalezaji wa mradi huo,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Bosco Komba amesema,halmashauri hiyo itaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha miundombinu hiyo inalindwa na kutunzwa ili kuimarisha utoaji wa elimu bora na endelevu.

Kwa upande wake mkazi wa Kata ya Iwindi,Juma Abdallah amesema,wananchi wanatambua thamani ya uwekezaji huo na wamejipanga kuilinda miundombinu ya shule dhidi ya uharibifu wowote.

“Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa shule hii,sisi wananchi tutahakikisha inalindwa ili iendelee kuwahudumia watoto wetu na vizazi vijavyo,”amesema Abdallah

k