



Na Joyce Kasiki,Timesmajira Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, ametembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na kuipongeza taasisi hiyo kwa namna inavyotekeleza majukumu yake.
Ridhiwani ametoa pongezi hizo leo Juni 17, 2026, alipotembelea banda la EWURA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza Juni 16, 2026 na yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 25, 2026 katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.
“Hongereni sana kwa kazi kubwa mnayoifanya.”amesema Ridhiwani
Awali, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa EWURA, Hawa Mniga, almesema mamlaka hiyo inashiriki maadhimisho hayo kwa lengo la kuelimisha wananchi kuhusu shughuli na huduma zinazotolewa na taasisi hiyo.
“Tupo hapa katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kushughulikia kero na migogoro mbalimbali kuhusu masuala ya nishati ,” amesema Mniga.
Ameongeza kuwa ushiriki wa EWURA katika maadhimisho hayo unalenga kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo na kuwapa fursa ya kuwasilisha changamoto zao kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.

More Stories
Vijana wahimizwa kutumia fursa za kiuchumi
DCP Ngoso, DCF Ngenya na DCI Mwaifuge wajionea huduma Magerezani
VETA yathibitisha uwezo kwa mhitimu mlemavu