May 15, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yatoa salamu nzito kwa Samia-Butiama

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Mara

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Mwenyekiti wake pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuheshimu na kuyaenzi matendo ya aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mei 15, 2026 na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, alipootembemea familia ya hayati Julius Nyerere ‘Baba wa Taifa’ nyumbani kwake Wilayani Butiama mkoa wa Mara.

Amesema, moja ya mambo ambayo Rais Dkt. Samia amekuwa akiyaishi matendo ya Hayati Nyerere ni pamoja na kukemea ubaguzi, kuhubiri juu ya masuala ya amani, mshikamano na ulmpendo na kueleza kuwa, yote hayo amekuwa akiyafanya pamoja na kuikumbuka familia ya muhasisi huyo kwa kuitembelea nyumbani kwake Butiama.

“Ninampongeza kwa dhati Rais Dkt. Samia kwa muda wote amekuwa karibu na familia hii ya Rais wetu wa kwanza kwani kila anapokuja katika mkoa huu lazima atembelee hapa nyumbani na hii inathibitisha kuwa, Rais wetu anaheshimu matendo mema ya Baba wa Taifa.

Lakini pia, Rais samia nae amekuwa akikemea majungu, maneno maneno, umbea, unafki na masuala ya shoti, kuaa isiwe sehenu yetu viongozi. Tuwe kitu kimoja na kuunganisha nchi, chama kwa maslahi ya wananchi”, amesema Kihongosi.

Aidha, Kihongosi ameendelea kusisitiza juu ya kulinda amani, akisema kuwa gharama za kurudisha amani iliyotoweka ni kubwa kuliko kuendelea kuilinda amani iliyopo.