Na Zena Mohamed,TimesmajiraOline,Dodoma
WIZARA ya Maliasili na Utalii imesema katika Mwaka wa Fedha 2026/2027 Wizara hiyo imejipanga kutekeleza vipaumbele tisa.
Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo Bungeni leo Mei 15,2026 Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Ashatu Kijaji amesema vipaumbele muhimu vyabutekelezaji ni moja kuimarisha uhifadhi, ulinzi, na matumizi endelevu ya rasilimali za wanyamapori, misitu, nyuki na malikale.
Mbili kuimarisha miundombinu wezeshi katika maeneo ya utalii na hifadhi ikiwemo barabara, viwanja vya ndege, mawasiliano na huduma za kijamii.
Tatu kuimarisha utangazaji utalii ndani na nje ya nchi kwa kutumia mikakati mahsusi ikiwemo masoko ya Mashariki ya Mbali na Mashariki ya Kati; ikiwemo kutumia fursa ya AFCON 2027, IPU, Mashindano ya ulimbwende ya dunia, utoaji wa tuzo za ubora kuhusu masuala ya utalii zinazoandaliwa na WTA matukio yatakayofanyika nchini.
Nne ni kuendeleza na kuboresha mazao ya utalii ya kimkakati ikiwemo utalii wa meli, mikutano na matukio (MICE), pamoja na kutambua na kusajili mazao mapya.
Tano kuimarisha uzalishaji, uongezaji thamani na masoko ya mazao ya misitu na nyuki.
Sita kuimarisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika usimamizi wa rasilimali, ulinzi, ufuatiliaji, ukusanyaji wa mapato, pamoja na utangazaji wa utalii;
Saba kuimarisha Utafiti, Ubunifu na Maendeleo ya Rasilimaliwatu.
Nane Kufanya mapitio ya Sera, Sheria, Kanuni na miongozo ili kuendana na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia na tisa ni kuboresha mazingira ya kazi, mifumo ya usimamizi wa utendaji na uwajibikaji.

More Stories
TAKUKURU Kinondoni yaainisha mafanikio Januari_ Machi 2016
Serikali yafikisha Umeme Katika Migodi 289 ya Wachimbaji Wadogo
Kichwa cha Marehemu James Temba Mwanafunzi wa IFM chapatikana