
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
Kamati ya fedha,utawala na mipamgo imewapongeza wananchi wa Kata Mkinga Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa kwa kuanzisha ujenzi wa kituo cha afya kwa nguvu zao wenyewe kwa kutoa mchango wa shilingi elfu tano kwa kila kaya.
kamati hiyo ikiogozwa na Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Joseph Mwenda, imetembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa kituo cha afya cha kata ya Mkinga kilichoanzishwa mwaka 2025 kwa nguvu za wananchi ndipo madiwani hao wakatoa pongezi hizo.

Miradi mingine iliyotembelewa na kukaguliwa kamati hiyo ni pamoja na ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa shule ya sekondari Usesula kupitia mradi wa Boost wenye thamani ya Tshs,Mil.20.5 na ,ukarabati wa mabweni shuleni ya sekondari kipili kupitia serikali kuu Tshs,Mil.40,ujenzi wa vyoo matundu nane shule ya msingi katongolo kupitia mapato ya ndani Tshs,Mil.10 ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na vyoo matundu sita na shule ya msingi kirando kupitia mradi wa Boost Tshs,Mil.88 .
Awali akisoma taarifa ya mradi huo mtendaji wa kata ya Mkinga Victor Lagita alisema mradi huo umeanzishwa kwa nguvu za wananchi kwa kuchangia kila kaya shilingi elfu tano ili kuwezesha ujenzi huo.
Alidai kuwa Wananchi walisukumwa na hari hiyo baada ya kipindi kirefu kufuata huduma hizo mbali hasa katika Kituo Cha afya Kirando na kuwa njia pekee na sahihi kwao ni kuamua kutumia nguvu zao kuanza ujenzi wa Kituo hicho Cha afya.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mkinga Mohamed Issa Zaidi ameiomba serikali kuwashika mkono na kuunga juhudi za ujenzi huo ili wananchi waweze kupata majengo mengi na huduma bora katika mwambao wa ziwa Tanganyika.
Amesema kuwa yeye kama Diwani kwa kushirikiana na viongozi wenzie wa vijiji wamekubaliana kuwa Kila kitu kinachofanyika kuwa wazi kwa Wananchi na kusomewa mapato na matumizi ya michango Yao na kuwa hiyo itaondoa manung’uniko na kuwatia moyo Wananchi na kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia Watu kutovinjika moyo na kuendelea kujitoa na kuweza kulifikia lengo.

Wananchi kwa upande wao wamedai kuwa wao kwa Sasa hawapo tayari kukwamishwa na jambo lolote kwani lengo lao ni kupata Kituo Cha afya na kuwa wamechelewa kwa muda mrefu kupata Kituo Cha afya na kuwa wao walidhani kuwa Serikali pekee ndiyo yenye jukumu la kuwajengea Kituo Cha afya kumbe inawezekana hata kwa nguvu zao na kuwa ni rahisi kwa Serikali kuunga mkono juhudi hizo kwa kusaidia baadi ya vitu ikiwemo kupaua nk.


More Stories
MWADETA yahamasisha matumizi ya folic acid
Chanjo ya polio awamu ya pili kuwafikia 176,644
DC ubungo awaasa zimamoto kushirikiana na wadau wengine