Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Benki ya NMB Plc imeendelea kuthibitisha ubora wake katika masuala ya usalama mahali pa kazi, ustawi wa wafanyakazi na ufanisi wa kiutendaji baada ya kutwaa tuzo tano katika Tuzo za Kitaifa za AOSH kwa mwaka wa pili mfululizo.
Tuzo hizo zilizofanyika chini ya kaulimbiu isemayo “Mazingira Bora ya Kazi Kisaikolojia: Njia ya Wafanyakazi Kufanikiwa na Taasisi Imara”, zililenga kutambua taasisi zinazojenga mazingira salama, yenye afya na yanayowajali wafanyakazi.

Katika tuzo hizo, NMB ilishinda tuzo ya Proactive Capital – Safety Investment Award, ikionesha juhudi zake za kuwekeza katika usalama wa wafanyakazi, kuzuia hatari na kulinda ustawi wa rasilimali watu.
Aidha, benki hiyo ilishika nafasi ya pili (First Runner-Up) katika kipengele cha Financial Administration kutokana na usimamizi mzuri wa fedha na viwango vya juu vya uendeshaji wa taasisi.

NMB pia ilipata nafasi ya pili katika kipengele cha Inclusion & Support Award, huku tawi la NMB Clock Tower likishika nafasi ya pili katika kundi la Financial Activities.

Vilevile, benki hiyo ilipata nafasi ya tatu (Second Runner-Up) kwa juhudi zake za kusaidia na kuwajali wafanyakazi wenye ulemavu, jambo linaloonesha dhamira yake ya kujenga mazingira jumuishi yanayowawezesha wafanyakazi wote kufanya kazi kwa ufanisi na kujiamini.


More Stories
Mchengerwa akabidhi boti za kuimarisha huduma za chanjo
Baobab wakutana na NBAA wapatiwa elimu ya Uhasibu
Waziri Ndejembi,Dkt.Ramokgopa wakubaliana kuimarisha Ushirikiano wa Nishati