Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Zaidi ya wanaume 2,000 mkoani Mwanza,wanatarajia kushiriki katika kongamano la wanaume(wanaume summit 2026), lenye lengo la kuibua mjadala mpana kuhusu nafasi, changamoto na mustakabali wa mwanaume katika jamii ya kisasa.
Kongamano hilo ambalo linafanyika kwa takribani mara ya 56, limeandaliwa na taasisi ya Wanaume Tanzania (Men at Work Global) pia katika tukio hilo taasisi hiyo itakuwa inaadhimisha miaka 11 ya gu kuanzishwa kwake(2015-2026).
Akizungumza Aprili 25,2026 na Waandishi wa Habari mkoani Mwanza,Rais na Mwanzilishi taasisi ya Men at Work Global,Maxwell Shing’oma,amesema kongamano hilo litafanyika Aprili 2026, jijini Mwanza.
Ambapo anaamini kupitia kongamano hilo sauti ya mwanaume itasikika kwa upana zaidi na kuchochea mabadiliko chanya katika jamii.
Maxwell amesema, kongamano hilo litawakutanisha wanaume kutoka makundi mbalimbali ya kijamii.Pia aliwakaribisha wanawake kushiriki ili kujenga uelewa wa pamoja na mshikamano katika familia na jamii kwa ujumla.
Pia amesema,katika kipindi chote, taasisi hiyo imefanikiwa kuwafikia maelfu ya watu kupitia semina, makongamano na programu mbalimbali zilizofanyika maeneo ya shuleni, taasisi na vyuo vikuu.
Sanjari na hayo amesema,taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya malezi, uongozi na maendeleo binafsi kwa vijana na watu wazima, ikiwa na lengo la kujenga jamii yenye wanaume wanaojitambua na kuwajibika.
“Katika kongamano hili kutakuwa na mada mbalimbali ikiwemo afya ya akili,ambazo zitatolewa na Joram Nkumbi,Timoth Kyara,Sam Salali,Shemeji Melayeki na Charles Ndutu,litafanyika ukumbi wa chuoa cha Benki Kuu Tanzania(BOT),”amesema Maxwell.

More Stories
Watumishi NIRC washerehekea mwaka 2026,waaswa kuimarisha mshikamo,uwajibikaji
ACT Wazalendo yaingia mazungumzo ya kisiasa kwa maslahi ya Zanzibar na wananchi wake
Chongolo, azindua kampeni ya “Linda Ushirika, Chagua Uadilifu”