Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Benki ya NMB imetunukiwa cheti cha hadhi ya Superbrand Afrika Mashariki kwa kipindi cha 2026–2028 baada ya kupata kura nyingi zaidi za watumiaji katika kundi la benki, kwa mujibu wa Baraza la Superbrands.
Utambuzi huo umetokana na tathmini iliyohusisha Baraza la Superbrands na watumiaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Miongoni mwa vigezo vilivyotumika ni ubora wa bidhaa na huduma, utofauti wa chapa pamoja na uwezo wa kutoa huduma kwa kiwango kinachofanana kwa muda.

Mjumbe wa Baraza la Superbrands, Dorine Bangapi, amesema hadhi hiyo haiwezi kununuliwa, kwa kuwa uteuzi hutokana na maoni na kura za watumiaji. Amesema NMB ilipata kura nyingi zaidi katika kundi la benki.
Cheti hicho kilipokelewa kwa niaba ya NMB na Mkuu wa Idara ya Masoko, Rahma Mwapachu. Benki hiyo imesema utambuzi huo unaongeza wajibu wa kuendelea kuboresha huduma na kulinda imani ya wateja wake.

More Stories
NMB yaingia 10 Bora Duniani
Yas yaboresha mazingira ya elimu Buigiri, Dodoma
Waziri Salome ashiriki ufunguzi Gastech 2026 Bangkok