November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ZYBA kuwapiga msasa makocha, waamuzi

Na Angela Mazula, TimesMajira Online

TAASISI ya Young Basketball Association (ZYBA) imeandaa mkakati wa kutoa mafunzo kwa waamuzi, makocha na viongozi wa klabu mbalimbali za mpira wa kikapu utakaoanza kutekelezwa rasmi mwanzo ni mwa mwaka 2021.

ZYBA imekuja na mpango huo baada ya kupata mafanikio makubwa katika program maalum ya mafunzo ya muda mrefu ya mpira wa kikapu kwa vijana wenye umri wa miaka 15-25 ya ‘Learn Basketball Skills With ZYBA’ iliyodumu kwa takribani miezi miwili.

Katika mafunzo hayo yaliyozinduliwa Agosti 8 zaidi ya vijana 180 ambao baadhi yao walitokeo katika klabu mbalimbali walinufaika na mafunzo hayo.

Vijana ambao walitoka katika timu kwa sasa wanaendelea na mafunzo chini ya makocha wao laki ni pia 18 wamekabidhiwa kwa klabu ya New West ili kuendelea kujinoa zaidi na kufikikia malengo waliyonayo katika mchezo huo.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Aziz Salim amesema, baada ya kuona mafunzo hayo yamekuwa na manufaa, mkakati uliopo ni kuwageukia waamuzi, makocha na viongozi wa klabu.

Lakini mbali na kundi hilo pia watakuwa na mafunzo ya muda mfupi kwa vijana kwa lengo la kuwajenga zaidi ili kuwa bora katika siku za mbeleni.

“Tunashukuru kuwa mafunzo tuliyoyaendesha yameonesha manufaa makubwa na tayari baadhi ya vijana ambao tulikuwa tukiwapa mafunzo tumewanganisha na baadhi ya timu ambazo zinafanya mazoezi kila siku ili kupata ushindani na kukuza viwango vyao na tunaamini watakuja kuwa wachezaji bora zaidi ambao faida yake tutakuja kuiona siku za mbeleni,” amesema Mkurugenzi huyo na kuongeza.

“Mafanikio haya ndiyo yaliyotufanya tuja na programu nyingine kwa vijana ambayo itakuwa ya muda mfupi lakini pia tumeshaweka mpango wa kuanza mafunzo kwa waamuzi, makocha na viongozi ili kuwapa uzoefu zaidi,”.