May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jadon Sancho

Tetesi za soka Ulaya leo Jumatatu tarehe 19.10.2020

Jadon Sancho

Manchester United imepewa matumaini kuwa inaweza kusaini mkataba na winga wa Borussia Dortmund raia wa England Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 20, baada ya ‘kumuhukumu vibaya’ alipomtaka msimu uliopita. (Star)

United pia wanamlenga kiungo wa kati wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 16 Luis Gomes. Kiungo huyo wa safu ya kati Mreno amepewa jina la ‘ Luis Figo’ ajaye nchini mwake. (Mirror)

Adama Traore

Winga wa Wolves Adama Traore, mwenye umri wa miaka 24, yuko tayari kupokea wito katika klabu ya Barcelona na Liverpool ili kusaini mkataba mpya wa pauni 100,000-kwa wiki katika Molineux.

Mshambuliaji huyo wa Uhispania alijiunga na klabu hiyo akitokea Middlesbrough mwaka 2018. (Sun)

Hiyo inakuja baada ya Liverpool kushauriwa itafute mchezaji wa kuziba pengo la Virgil van Dijk

Hata hivyo, Mlinzi wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher anasema klabu hiyo lazima imsaini kiungo wa safu ya kati-nyuma baada ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Virgil van Dijk, menye umri a miaka 29, kupata majeraha wakati wa mechi yao dhidi ya Everton. (Mail)

Winga wa Liverpool Harvey Elliott, mwenye umri wa miaka 17, alikitathmini kikosi cha Blackburn kabla ya kukubali uhamisho wa mkataba wa deni katika upande wa Championi.(Mail)

Wyne Rooney

Mchezaji na kocha wa Derby County Wayne Rooney, mwenye umri wa miaka 34, anatarajia kupata matokeo ya vipimo vya Covid-19 test, baada ya kugundua kuwa rafiki yake aliyemuuzia saa ya mkononi alikuwa na virusi vya corona. (Daily Telegraph – subscription required)

Klabu za EFL zinatishia kuzuwia jaribio la kulipa ushuru ili kupata dhamana ya serikali . (Sun)

Paulo Dybala

Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 26, alikuwa na malumbano na afisa mkuu wa soka wa Juventus Fabio Paratici baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichoingia uwanjani Jumamosi. (Mail via Tuttosport)

Naye kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, pia analengwa na Barcelona. Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 29, yuko mwaka wa mwisho wa mkataba wake na msimu ujao atakuwa huru. (AD, via Sky Sports)

Allan Saint-Maximin

Winga Mfaransa Allan Saint-Maximin, mwenye umri wa miaka 23, alikuwa mmoja wa wachezaji wa Newcastle wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi aliposaini mkataba mpya wa miezi sita- ambapo malipo yake yaliongezeka mara dufu hadi kufikia pauni 70,000 kwa wiki. (Newcastle Chronicle)

%%%%%%%%%%%%%%%