May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zungu akemea mgambo kunyanyasa Bodaboda, Mama Lishe

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ameitaka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam isiwanyanyase Boda boda na wafanyabiashara wa mama lishe wanaofuata taratibu za Usafi .

Mbunge Zungu amesema hayo katika kikao cha Utekelezaji wa ILANI Jimbo la Ilala ambapo amesema mgambo wa Halmashauri hiyo wanawanyanyasa waendesha pikipiki maarufu Bodaboda kwa kiwakamata na kuwatoza faini bila risiti na kudaiwa kumwaga vyakula vya vya mama lishe .

“Kuanzia leo Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary KUMBILAMOTO sitaki mgambo wanyanyase wamachinga na mama lishe kuwamwagia vyakula vyao wakati wanaofuata sheria za usafi na Bodaboda wanakamatwa wanatozwa faini bila kupewa risiti Ilala ” amesema Zungu .

Mbunge Zungu aliwataka mgambo wa Ilala wafuate sheria waache kufanya uonevu kwa wafanyabiashara Ilala ambao wanajishughulisha na kujipatia kipato .

Katika hatua nyingine Mbunge Zungu alisema mgombea urais 2025 Tanzania kwa tiketi ya CCM Samia Suluhu Hassan, katika Uongozi wake amefanya mambo makubwa nchini kwa utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ambapo baadhi ya miradi aliyotekekeza katika Uongozi wake wa serikali ya awamu ya sita sekta ya afya ,Elimu ,miundombinu ya Barabara miradi mkakati ikiwemo Reli ya kisasa SGR ,bwawa kufufua umeme yote amesimamia.

Pia ametumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wa Jimbo la Ilala Madiwani ,Wajumbe wa shina ,Wenyeviti serikali za Mitaa viongozi wa Wilaya Mkoa na Viongozi wa Taifa Kwa kumpa ushirikiano katika Uongozi wake ambapo Ofisi ya Jimbo la Ilala ilitoa vyeti vya kuwatambua mchango wao.

Katibu wa CCM mkoa Dar es Salaam Adam Ngarawa amewatoa shaka Watanzania kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Rais makini.

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Omary KUMBILAMOTO amempongeza Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa za miradi ya Maendeleo wilayani Ilala na Jimbo la Ilala kwa ujumla Katika miradi ya elimu ,afya ,barabara .

Kwa upande Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Dar es Salaam Abas Mtemvu, amesema Madiwani na Wabunge katika Mkoa Dar es Salaam wasiofanya kazi za Utekekezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) wakitegemea pesa zao wasichaguliwe badala yake amewataka wananchi wawachague wale wanaotekeleza Ilani na kutatua kero za wananchi .

“Kazi ya Diwani unapochaguliwa ukingia halmashauri kutafuta miradi ya maendeleo katika kata yako na kazi ya Mbunge kutafuta miradi katika jimbo lako Ili kuleta maendeleo na kutatua kero za wananchi waliokuchagua ndio sehemu ya kipimo chako katika Mkoa wangu wa Dar es Salaam amna udiwani wa pesa na ubunge wa pesa utapimwa kutokana na kazi zako za Utekekezaji wa Ilani na kuwatumikia wananchi ” amesema Mtemvu.

Mwenyekiti Mtemvu aliwataka Madiwani na Wabunge kujishughulisha katika kutafuta miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi .

Aidha amewataka kusimamia miradi ya maendeleo ambayo imetelezwa na Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muunguno wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan, ikiwemo miradi ya Afya ,Elimu na miundombinu ya Barabara .

Akizungumzia Jimbo la Ilala Mtemvu amewataka wana Ilala watumie nafasi ya Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu, waitumie vizuri badala yake wasichezee katika kushirikiana kuleta maendeleo wilayani Ilala ikiwemo Utekelezaji wa Ilani.

Wakati huo huo Mtemvu amesema katika Miaka yake mitano ya uongozi kila mwendesha boda boda Mkoa Dar es Salaam aweze kumiliki piki piki yake waweze kupata fursa wasimiliki boda boda za matajiri wao.