Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo fleva kutoka WCB anayefanya vizuri hapa nchini, Zuhura Othman Soud maarufu kama ‘Zuchu, amefarijika sana kuwasaidia baadhi ya Kinamama waliopo mji mpya wa Kwahani kibanda hatari Kisiwani Unguja.
Akizungumza kwa faraja mara baada ya kutimiza zoezi hilo Zuchu amesema, kuna msemo unaosema ‘Poverty has a Woman Face’,ukiwa na maana umaskini una sura ya mwanamke jambo ambalo limemuumiza sana.
“Nikiwa kama binti, msemo huu unaniuma kweli kweli japo hatuwezi kukwepa, tathmini ya changamoto hii duni inayowakabili wanamama. Ila Kama binti pia najihisi nina jukumu japo lakusaidia kidogo kupunguza hali hii.
“Ni jukumu langu kama mwanamke lakini pia kama mtoto ninaejua changamoto wanazopitia wanawake kwenye kujikwamua kiuchumi.Jana Mlijitokeza kwa wingi na nilitamani kumgusa kila mmoja Wenu, Kwa kidogo nilichofanikiwa kugawana nanyi,namuomba Mwenyezi Mungu atupe uhai na rizki Ilituweze kuendeleza hili tulolianza jana la Kuinuana .
“Sijawahi kufanya Jambo nikafarijika na kujawa na Amani Kama baada ya Jana. Wallahi ‘My heart is Full of joy’. M/MUNGU akawainulie mitaji yenu na awakuzie vipato vyenu.Ameen,” amesema Zuchu .
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio