December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ziara ya mawakala wa Utalii kutoka Zanzibar kutembelea hifadhi ya Taifa Saadan

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wawakilishi 20 wa Umoja wa Mawakala wa Utalii Zanzibar “ZATO” wamefanya ziara ya siku tatu mwishoni mwa wiki kutembelea Hifadhi ya Taifa Saadani.

Lengo la ziara hii ni kuona vivutio na shughuli za utalii zilizopo hifadhini pamoja na fursa za uwekezaji.

Mategemeo ni kuwa na ushirikiano ambao utaongeza idadi ya wageni na wawekezaji katika Hifadhi ya Taifa Saadani.

Mawakala wa Utalii wa Zanzibar wameahidi kuitangaza Saadani katika masoko yao na kuingiza Saadani kwenye Safari
package kwa wageni.

Mapendekezo/ushauri waliotoa ni pamoja na Saadani kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara za utalii ndani ya hifadhi, kuongeza idadi ya wanyamapori na kuhakikisha michezo mbalimbali ya kwenye maji (bahari na mto wami) inaongezeka.