January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ziara ya Balozi wa Marekani nchini Hospitalini CCBRT katika picha

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Balozi Donald J. Wright M.D (kushoto) akijadiliana jambo na Mtaalamu wa kutengeneza macho bandia, Rehema Semindu (kushoto) wakati wa ziara yake ndefu aliyoifanya hospitalini hapo siku ya Jumanne wiki hii. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospital ya CCBRT, Brenda. Katika ziara hiyo, Balozi huyo wa Marekani alitembelea vitengo mbalimbali pamoja na jengo jipya litakalo hudumia watoto na akina mama wenye ujauzito hatarishi. Aliambatana pia na Sophia Nur – Mkurugenzi Mshirika wa Mawasilianona Sera – CDC, Gene Peuse – Mshauri Mwandamizi wa Ubia- USAID Tanzania na Carrie Cafaro – Mkuu wa Utekelezaji wa Programu – Vodafone USAID.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi (wa pili kulia) akimkaribisha Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Balozi Donald J. Wright M.D ambaye alifanya ziara ndefu ya kujionea kazi kubwa ambayo inafanywa na hospital hiyo sambamba na kutembelea vitengo mbalimbali pamoja na jengo jipya litakalo hudumia watoto na akina mama wenye ujauzito hatarishi. Katika ziara hiyo, Balozi Wright aliambatana na Sophia Nur – Mkurugenzi Mshirika wa Mawasilianona Sera – CDC, Gene Peuse – Mshauri Mwandamizi wa Ubia- USAID Tanzania na Carrie Cafaro – Mkuu wa Utekelezaji wa Programu – Vodafone USAID.