November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zaidi ya bili 1 zatumika kuelimisha makuzi ya Albino nchini


Na Rose Itono

SHIRIKA linalojishughulisha na kutoa huduma za kielimu na kiafya kwa watu wenye ualbino
la Inside The Side lenye Makao Makuu yake Nchini Uholanzi limeanza programu maalumu ya kutoa elimu kwa vijana nchini Ili kuwawezesha kukua wakijua malezi na makuzi ya watoto wenye ualbino

Akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Desiree Schoonen alisema, elimu hiyo itatolewa mashuleni na vyuoni kwa njia ya hadithi kupitia filamu iitwayo White Berry

Amemtaja mhusika Mkuu kwenye filamu hiyo kuwa ni Latifa Mwazi ambaye naye pia alizaliwa akiwa albino mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

” Filamu hii itakuwa ni mahususi kwa ajili ya kuelimisha Jamii kuhusu malezi na makuzi ya watu wenye ualbino na tumeanzia mashuleni na vyuoni Ili kundi rika hili liweze kukua na kutambua kuwa kila binadamu ana haki za msingi ikiwa ni pamoja na kuishi,’ alisema Schoonen na kuongeza kuwa elimu hii ni mwanzo lakini lengo ni kufikia nchi nzima

Amezitaja baadhi ya shule na vyuo ambavyo vitafijiwa na elimu hiyo katika awamu ya kwanza kuwa ni pamoja na shule ya msingi St Anne Maria ya Mbezi Jijini Dar es Salaam, Chuo Cha UDOM,KCMC Moshi na IAA Cha Arusha.

Schoonen ameishukuru ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania kwa kufadhili.kila hatua ambayo imefanikisha kukamilika kwa filamu hiyo ambapo mpaka kukamilika kwake zaidi ya Sh. Bilioni 1 zimetumika

Kwa upande wake mhusika Mkuu kwenye filamu hiyo Latifa Mwazi amesema kutokana na Jamii kunyanyapaa watu wenye ualbino ameamua kuwa balozi kwa kuandaa filamu hii Ili ielewe kuwa ualbino siyo umasikini badala yake ni binadamu kama wengine na anaweza kufikia mbali na kuwataka wazazi na walezi kuacha kuwafungia ndani watoto wenye ualbino badala yake wawapeleke shule Ili kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Ameongeza kuwa kutokana na elimu aliyoipata kuhusu haki za albino hajutii kuzaliwa albino kwani mpaka.sasa anaishi maisha mazuri na tayari amekuwa raia wa Uholanzi

“Mwanzo ulikuwa mgumu sana kwangu nilijijatia tamaa nikawa najiina wa tofauti lakini sasanimetambua albino ni binadamu kama wengine na akipatiwa haki zote za msingi kama.binadamu wengine anaweza kufika mbaki kiuchumi na hata kwenye uongozi,” amesema Mwanzi

Ameongeza kuwa filamu hii kwa Sasa imeanza kuoneshwa mashuleni na vyuoni lakini mapema mwakani itaanza kuoneshwa kwenye Mabasi ya mikoani Ili kila mtu akiwa safarini aweze kupata elimu hii

” Filamu hii kwa Sasa inaoneshwa kwa lugha ya kigeni lakini hadi kufikia.mwakani itakuwa imetafsiriwa kwa lugha ya taifa Ili kila.Mtanzania aweze kuelewa kinachosimuliwa na kuwa balozi kwa mwingine

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Mabasi Tanzania ( UWAMATA) Majura Kafumu ameushukuru uongozi wa Shirika la Inside The Side kwa kuona umuhimu wa filamu hii kuoneshwa ndani ya Mabasi ya mikoani kwani kufanya hivyo Jamii kubwa itaelimika

” Kuoneshwa kwa filamu hii ndani ya Mabasi yaendayo mikoani kutasaidia kuelimisha janiii kutambua kuwa watu wenye ualbino ni ndugu zetu, na wana haki kama binadamu wengine na wanaweza kufika mbali endapo wakipatiwa malezi bora kutoka kwa wazazi, walezi na Jamii

Pia amesisitiza kuiasa jamii kuacha tabia za kuhusisha kundi hili na Imani za kishirikina kwani kufanya hivyo ni kosa ambalo linaweza kusababisha kupoteza haki zao za kimsingi ikiwepo elimu na afya

Hata hivyo amesema elimu hiyo kwa vijana ambao ni kundi rika itawezesha kutengeneza kizazi bora chenye kupinga unyanyapaa dhidi ya watu wenye ualbin