Na Mwandishi Wetu,timesmajira,Online
SERIKALI kupitia kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, mapema leo Septemba 17,2021 imeingia makubaliano ya kutangaza Utalii wa Tanzania kupitia Mlima maarufu Duniani, Mlima Kilimanjaro pamoja na Visiwa vya Zanzibar kwa kuweka nembo katika jezi zake kuelekea michezo ya Kimataifa ambapo imefanya hivyo pasipo malipo.
Akizungumza katika tukio hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ameipongeza timu ya Yanga kwa kuleta wazo hilo la kuutangaza Utalii wa Taifa, kupitia safari zake za Kimataifa katika mchezo wake wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United FC ya nchini Nigeria na michezo mingine kama itafanikiwa kufuzu raundi inayofuata.
“Timu ya Yanga wameweka nembo ya Mlima Kilimanjaro, visiwa vya Zanzibar katika Jezi zao zote, ili kutangaza utalii wa Tanzania bure kabisa bila hata malipo
Lakini kama wangetaka pesa basi ingekuwa zaidi ya Bilioni1 za Kitanzania kuweka nembo hii kwenye jezi hizo” amesema Dkt. Ndumbaro.
Hatua hiyo inakwenda sambamba na juhudi za Rais wa Tanzania, . Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii wa nchi kupitia kipindi maarufu cha Royal Tour alichokianzisha yeye mwenyewe.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Timu ya Yanga, Haji Mfikirwa amesema Yanga inafanya hayo yote kuunga mkono jitihada za Tanzania kuendelea kutangaza utalii wake, na kwamba hiyo ni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mashabiki ndani na nje ya nchi kitendo kinachoweza kuvutia idadi kubwa ya Watalii duniani.
More Stories
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha