Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MSANII wa filamu na Mjasiriamali hapa nchini Jackline Wolper, amewataka wanawake kufanya kazi kwa bidii ili waweze kupata kipato na kupiga hatua katika maisha.
Akitoa ushauri huo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Wolper amesema, mwanamke akisimama vyema anaweza kutajirika hata kupitia kwa mtu lakini anatakiwa kufanya kazi kwa bidii kutimiza malengo yake.
“Mwanamke wa leo unayewaza kutajirika kupitia M2 (kijeba,jemba), Dada yangu amka fanya kazi, fanya biashara,tafuta kazi usichague kazi, acha dharau, acha uwoga, usiangalie m2 usoni kwamba nani atasemaje na watakuchukuliaje, fanya kazi yoyote isiyodhuru uwahi wako,” amesema Wolper.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA