November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wizara ya Madini yajipanga kukusanya Bilioni 650/-

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira,Online- Maelezo, Dodoma

NAIBU Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya amesema Wizara hiyo imejipanga kuhakikisha malengo ya kukusanya sh. Bilioni 650 katika mwaka wa fedha 2021/22 yanafikiwa kwa wakati kutokana na mikakati iliyowekwa.

Ameyasema hayo jana Jijini Dodoma wakati wa Semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini inayolenga kuwajegea uwezo wajumbe hao ili waweze kutekeleza jukumu la Kuisimaia sekta hiyo kikamilifu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dastun Kitandula , akizungumza wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jana Jijini Dodoma.

“Tumejipanga kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwaa yanafikiwa na tunavuka kwa ushauri na maoni yatakayotolewa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini tunaamini kwa pamoja tutaweza kuongeza mchango wa sekta ya madini na kukuza zaidi mchango wake katika kukuza uchumi”, amesisitiza Prof. Manya

Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya akieleza mikakati ya Wizara hiyo katika kuendelea kukuza sekta ya madini hapa nchini wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika jana, Jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dastun Kitandula amesema kuwa wajumbe wa Kamati hiyo wamejengewa uwezo na uwelewa kuhusu sheria ya Madini ya mwaka 2017, mfumo wa utoaji leseni za uchimbaji na utafiti wa madini na ushiriki wa Watanzania katika sekta ya madini.

Mwanasheria kutoka Tume ya Madini, Khadija Ramadhani akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jana,Jijini Dodoma.

Akifafanua zaidi, Kitandula amesema kuwa wajumbe wa Kamati hiyo wamepata uelewa wa kutosha kuhusu ushiriki Watanzania na faida wanazopata kutokana na sekta ya madini kusimamiwa vizuri baada ya kufanyika kwa mageuzi makubwa yanayotoa fursa kwa Watanzania kunufaika na rasilimali madini.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi, Yahya Samamba amesema kuwa pamoja na malengo mengine semina hiyo inalenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kuwasaidia katika kuelimisha wananchi katika maeneo yao na pia kuisimamia sekta hiyo .

Semina ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imefanyika Jijini Dodoma jana na kushirikisha wabunge ambao ni wajumbe wa Ka