Na Rose Itono,Timesmajira
WAZIRI wa Ujenzi Abdalah Ulega anatarajia kufungua semina endelevu ya wataalamu wa sekta ya Ujenzi iliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) ambapo mada kuu itakuwa ni kujenga utaalamu endelevu wenye viwango na mikakati.
Akuzungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam leo Juni 23 Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Mbunifu Daniel Matondo amesema, semina hii ni utekekezaji wa jukumu la kisheria la kuhakikisha wataalamu wa sekta ya Ujenzi wanaendelea kuboresha ujuzi na maarifa yao.
Amesema elimu hii huwezesha wataalamu waliosajiliwa na bodi kutimiza vigezo vya sheria na kitaaluma vinavyohitajika kwa ajili ya usajili endelevu Mbunifu Majengo Matondo amesema mada Kuu kwenye semina hiyo itakuwa ni Kujenga utaalamu endelevu, Viwango na Mikakati ambapo kwenye mada hii bodi itahakikisha wataalamu wake wanajengewa uwezo
” Mada hii inaakisi dhamira ya AQRB katika.kuhakikisha kuwa wataalamu wake wanajengewa uwezo si tu katika fani zao bali pia katika maeneo muhinu yanayochangia mafanikio na ustahimilivu wa taaluma zao,” amesema Mbunifu Majengo Matondo
Amesema katika.mada hii kutakuwa na mada ndogondogo tatu ambazo zitawasilishwa na kujadiliwa ikiwepo ya mikakati ya biashara na Usimamizi wa fedha kwa wataalamu wa sekta ya ujenzi
” Mada hii inalenga kuwawezesha wataalamu kuwa na ujuzi wa uendeshaji wa biashara, utunzaji wa kumbukumbu, ushuru na uthibiti wa fedha kwa ufanisi,” amesema Mbunifu Majengo Matondo
Ametaja mada ingine ndogo kuwa ni kujumuisha mienendo endelevu katika ubunifu na Usimamizi wa Majengo ambayo hi utajadili mbinu za kuhakikisha majengo yanabuniwa kwa kuzingatia mazingira, matumizi bora ya nishatiusalama na uimara wa muda mrefuIngine ni mabadiliko muhinu katika sheria ya AQRB Namba 4 ya mwaka 2010 pamoja na kanuni zake za mwaka 2024, mada hii ni ya msingi kwani inatoa ufafanuzi wa mabadiliko yaliyofanyika na athari zake kwa wataalamu wote waliosajiliwa na bodi
Amesema zaidi ya wadau 700 wanatarajiwa kushiriki kwenye semina hiyo ambayo itafanyika Juni 25 Jijini Dar es Salaam.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako