April 24, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya Access Tanzania yapanua huduma zake nchini, yaimarisha huduma za kibinafsi na biashara

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

BENKI ya Access nchini imetangaza rasmi kukamilika kwa mafanikio ya ununuzi wa kitengo cha Huduma za Wateja wa Kawaida, Binafsi na Biashara cha Benki ya Standard Chartered Tanzania, baada ya kukamilika kwa taratibu zote muhimu za kisheria na kupokelewa kwa idhini kutoka kwa mamlaka husika za udhibiti.

Hatua hii inaashiria mafanikio makubwa katika safari ya mageuzi ya Access Bank Tanzania kama benki ya biashara kamili inayolenga utoaji wa huduma jumuishi, salama, na za kidijitali kwa watu binafsi, wajasiriamali, na wafanyabiashara nchini kote.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari,imesema uunuzi huu hauhusiani tu na upanuzi wa huduma bali ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yetu ya kuwafikia Watanzania wengi zaidi kwa huduma za kibenki za kiwango cha kimataifa zinazoweka mteja mbele, amesema Imani John, Mkurugenzi Mtendaji wa Access Bank Tanzania.

Amesema kwa kuchanganya uzoefu wa Standard Chartered katika huduma za kifedha na mtazamo wa kidijitali unaoongozwa na Access Bank pamoja na mtandao wetu barani Afrika, tunajenga jukwaa madhubuti la uwezeshaji wa kifedha kwa wote.

“Kupitia ununuzi huu, Access Bank Tanzania imeongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wake wa kuwahudumia Watanzania, na kuchangia kwa dhati ajenda ya taifa ya ujumuishaji wa kifedha. Benki sasa itaweza kutoa huduma zilizobuniwa mahsusi kulingana na mahitaji ya makundi mbalimbali ya jamii, yakiwemo watu wasiokuwa na akaunti benki, wenye kipato kikubwa, wamiliki wa biashara ndogo na za kati Akaunti za Biashara, wanawake na vijana,”amesema

Aidha faida kuu za ununuzi huu ni pamoja na huduma pana na Shirikishi,Huduma maalum kwa wateja wa thamani ya Juu,kuwezesha Biashara Ndogo na za Kati (Akaunti za Biashara)Kupitia jukwaa la PrimusPlus, Access Bank inapanua huduma za benki kwa Akaunti za Biashara, ikiwa ni pamoja na mikopo maalum, suluhisho za mtaji wa kazi, ushauri wa kifedha, na elimu ya fedha kwa ajili ya ukuaji wa biashara na kuunganika na minyororo ya thamani ya kikanda pamoja na kuinua Wanawake Kiuchumi, kuna uzoefu Bora kwa Mteja na Kuendeleza Ubunifu,”amesema

Amesema uchumi wa Tanzania una nguvu kubwa, lakini bado kuna Watanzania wengi ambao hawajafikiwa na huduma rasmi za kifedha.

“Muunganiko huu unatuwezesha kuwahudumia wateja wetu kwa ufanisi zaidi na kuwapa suluhisho ambazo si tu zinapatikana, bali pia zinawezesha,”amesema

Tunawakaribisha kwa moyo wote wateja wetu wapya kwenye familia ya Access Bank. Pamoja, tutaijenga Tanzania yenye ustawi wa kifedha kwa wote.