May 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Nyongo atembelea banda la Tume ya Madini Sabasaba

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametembelea Banda la Tume ya Madini na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Saalaam.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati mbele) akiwasili kwenye Banda la Tume ya Madini na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Saalaam.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho, amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imejipanga kuwawezesha wachimbaji wadogo ili wawe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa Sekta ya Madini.

Akielezea mikakati ya Serikali katika kuhakikisha Sekta ya Madini inakua zaidi amesema kuwa ni pamoja na kuhakikisha madini ghafi yanaongezewa thamani nchini kabla ya kusafirishwa nje ya nchi hivyo kuongeza ajira kwa watanzania.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akitoa maelekezo kwa washiriki wa maonesho wa Tume ya Madini.

“Kama Serikali tunataka kuhakikisha kuanzia mchimbaji, mchenjuaji, mwongeza thamani hadi mfanyabiashara wa madini ananufaika pamoja na watoa huduma kwenye shughuli za uchimbaji wa madini,” amesema Naibu Waziri Nyongo.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kutoka kushoto waliokaa mbele)akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Tume ya Madini.

Katika hatua nyingine Nyongo amewataka wachimbaji wa madini kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake.