Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kuzungumza na Uongozi wa Umoja wa Watu wenye Ulemavu waendesha Bajaji kutoka Mkoa wa Dar es Salaam (UWAWABADA) wametembelea katika ofisi yake jijini Dodoma kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujadiliana kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazowakabili katika sekta hiyo.
Aidha, Katika kikao hicho viongozi hao na wajumbe wa UWAWABADA wametoa pongezi zao kwa Waziri pamoja na Ofisi yake kwa namna wanavyo shughulikia masuala mbalimbali yanayowakabili Watu wenye Ulemavu ili kuimarisha ustawi wa kundi hilo.
More Stories
Tanzania ipo tayari kupokea wakuu wa nchi,mkutano wa nishati-Dkt.Kazungu
Chunya yafikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
HGWT yawarejesha kwao wasichana 88 waliokimbia ukeketaji