Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametembelea na kukagua maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara.
Akiwa katika ukaguzi huo, Waziri Ndalichako aliambatana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Mwita, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Ahmed, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dkt, Islam Seif, Katibu Mkuu wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Rajab pamoja na viongozi mbalimbali katika mkoa huo.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Ahmed amewataka Wananchi wa Mtwara na mikoa ya karibu kujitokeza kwa wingi Aprili Mosi katika uwanja wa Nangwanda Sijaona ili kuungana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2023 zinaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato