May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Mkuu mgeni rasmi Maadhimisho ya wahandisi

Na Jackline Martin, TimesMajira Online


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho ya 20 ya siku ya wahandisi
nchini, ambayo yatahudhuriwa na wahandisi 3,500.

Maadhimisho hayo ambayo yameandaliwa
na Bodi ya Usajili wa Wahandisi yataenda
sambamba na uapisho wa wahandisi wapya na kuwaingiza katika kundi la wahandisi mahiri


Akizungumza na waandishi wa habari jana
jijini Dar es Salaam, Msajili wa Bodi ya Usajili wa wahandisi, Injinia Bernard Kavishe, alisema maadhimisho hayo yatafanyika kesho Mliman city.


Alisema shughuli mbalimbali zitaanza
leo ikiwemo wahandisi kutoka kila pembe
ya Tanzania kukutana na kupata uzoefu wa eneo la mkutano.


Injinia Kavishe aliyataja malengo makubwa ya kuadhimisha siku hiyo ya wahandisi nchini kuwa ni kuiwezesha Jumuhiya ya kiuhandisi kuonesha umma nini wahandisi wa Tanzania wanafanya katika kuleta maendeleo ya nchi,
kuwatia moyo wanafunzi wa kitanzania
wanaosema uhandisi ili wafanye vizuri zaidi katika masomo yao na kuwaingiza katikabkundi la wahandisi wanafunzi


“Bodi kutoa mrejesho wa shughuli
zilizojiri kwa mwaka mmoja uliopita, Bodi
kupata mrejesho kwa wadau wa mambo
ya kipaumbele ya kushughulikia lakini pia
kupokea maelekezo kutoka kwa viongozi
wetu wa Afrika,” alisema.


Aidha Injinia Kavishe alizitaja shughuli
mbalimbali ambazo zitafanywa wakati wa
kuadhimisha siku ya wahandisi kwa mwaka huu 2023.


“Majadiliano ya kitaaluma na kiuhandisi,
kiapo cha wahandisi wataalamu, maonesho mbalimbali ya ubunifu, Teknolojia na biashara, kutoa tuzo mbalimbali kwa wahandisi na Makampuni yaliyoshamiri kwenye Sekta ya uhandisi, kuwatambua na kuwazawadia wahandisi wahitimu waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya mwaka wa mwisho (2021/2022) lakini pia kutakuwa na sherehe za ufunguzi na ufungaji”