December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Mkuu kuzindua program ya ujuzi Mbeya

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajia kuzindua programu ya kukuza ujuzi kwa vijana nchini awamu ya tatu baada ya serikali kupitia ofisi ya waziri Mkuu kudhamini vijana 14,440 kupitia vyuo 72 katika mikoa 26 ya Tanzania bara.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Juma Homera akizungumzia ujio wa Waziri Mkuu

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema jana Julai 31  mwaka huu  wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi  wa mafunzo ya uanagenzi awamu ya tatu yatakayofanyika kitaifa katika Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia (must) na Mgeni rasmi ni Waziri Mkuu.

Mhagama amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika Agosti 2 mwaka huu na kwamba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu imeelekeza nguvu katika  Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa programu ya kukuza ujuzi nchini kwa kuhakikisha inawafikia vijana wengi zaidi katika mikoa yote nchini ili kuzalisha wataalam katika nyanja mbalimbali serikalini

Akifafanua zaidi Mhagama amesema kuwa mafunzo hayo yanahusisha vijana kutumia asilimia 40 ya muda wao katika masomo ya nadharia huku asilimia 60 ikitumika katika masomo ya vitendo kama sehemu ya kazi.

“Ndugu waandishi wa habari mafunzo haya ya miezi sita yaliyoanza kutolewa mwezi Juni mwaka huu yanatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2021” amesema Waziri Mhagama.

Hata hivyo Waziri Mhagama ameeleza kwamba  tangu kuanzishwa kwa programu ya kukuza ujuzi kwa vijana mafunzo hayo yamefanyika kwa awamu mbili ambapo jumla ya  vijana 28,941 wamenufaika na kwamba awamu ya tatu imehusisha vijana 14,440.

Amesema kuwa Mkoa wa Mbeya  una jumla ya vijana 1,722  ambao wanapata mafunzo hayo kati ya vijana 14,440 wanaopata mafunzo nchini kwa kibali cha Rais  Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema kuwa kitendo cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuleta mafunzo hayo kuzinduliwa kitaifa mkoani Mbeya ni jambo la msingi Sana