Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Chita-Kilombero
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa leo anafanya ziara katika kikosi cha 837 Chita Kilombero mkoani Morogoro kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ya Kilimo na ufugaji inayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa katika kikosi hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari kikosini hapo Makamu Mwenyekjiti wa Kamati ya Kilimo mkakati,Mifugo na Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Peter Lushika,amesema lengo la ziara hiyo ni kujionea shughuli zinazofanywa na JKT kikosini hapo ambapo pia watapokea maelekezo yake ili kuboresha utendaji wa miradi mbalimbali wanayoitekeleza.
Aidha Kanali Lushika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi JKT amesema JKT inatekeleza miradi hiyo kwa weledi huku akisisitiza wanaendelea na kilimo cha mpunga katika shamba la Mngeta lililopo Mlimba mkoani Morogoro.
Naye Mkuu wa kikosi hicho Luteni Kanali Emmanuel Kukula amesema katika kikosi hicho kwa kushirikiana na Vijana wa JKT wanafanya shughuli za ufugaji wa samaki ikiwemo kutotolesha vifaranga vya samaki ambapo vijana wanafundishwa shughuli mbalimbali zikiwemo za ufugaji wa samaki kwa kugawanywa katika vikundi vidogo ili waweze kuelewa kile wanachofundishwa.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria