December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Aweso atoa maagizo DAWASA

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kushirikiana na wadau wengine wenye visima vikubwa vya maji kutoa huduma ya maji kwa kipindi chote cha ukame.

Akikagua zoezi la uunganishaji wa mabomba ya maji eneo la Wazo mkoani Dar es Salaam, Waziri Aweso amesema wizara yake itashirikiana na DAWASA kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji katika kipindi chote cha ukame.

Pia ameielekeza DAWASA kuzingatia vema ratiba ya mgao wa maji na kugawa maji bila ya upendeleoKwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA mhandisi Cyprian Luhemeja amesema, mradi wa maji ya visima wa Kigamboni wenye ujazo wa lita Elfu sabini utakamilika siku ya Jumapili na hivyo kuwawezesha wananchi kupata huduma ya maji.

Tarehe 25 mwezi huu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla alitangaza kuanza rasmi kwa mgao wa maji mkoani humo na katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Pwani, kufuatia kupungua kwa kina cha maji katika mto Ruvu.