Na David John,TimesMajira,Online Ludewa
WAZEE wa Kijiji cha Lugarawa,wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe wamempa baraka zote Mbunge wa Jimbo hilo Joseh Kamonga ambaye amepita bila kupingwa huku wakionyesha kukerwa na tabia ya kubadilisha wabunge Jimboni humo kila baada ya miaka mitano inapofika.
Wamesema kuwa hawapendezewi na tabia ya kila awamu ya uchaguzi kubadilisha Mbunge wa Jimbo hilo na kuwa mpya hali inayowacheleweshea maendeleo.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni za Mbunge huyo za kumuombea kura Rais Dkt John Magufuli ili kuwa kiongozi wa nchi kwa ngazi ya urais kwa awamu nyingine kampeni zilizofanyika Kijijini hapo.
Mmoja wa wanakijiji wa kijiji hicho Emmanuel Mtweve amesema kuwa wanamtaka mbunge huyo kwenda Bungeni kuwazungumzia wanaludewa .
“Tunakupa zawadi hizi za Mbuzi Dume na Kuku Jogoo kama ishara ya kukutaka kwenda kuwika Bungeni tena asubuhi mapema kwa ajili maendeleo ya nchi hii na zaidi ya watu wa Ludewa.”amesema Mzee Mtweve.
Nakuongeza kuwa .” Sisi wazee tunakupa zawadi hizi na tunaomba upokee ,kwanza tunakupongeza Sana kwa kupita bila kupingwa pamoja na kijana mwenzako wa kata hii ya Lugarawa Erasto Mhagama nendeni mkafanye kazi,”amesisitiza
Pia Mtweve amefafanua kuwa licha ya mambo mengine lakini zawadi hizi zinakwenda kumpa ujasili hata akiwa Bungeni kwenda kuzungumza changamoto wanazokumbana nazo wao.
Mbunge huyo wa Ludewa, Kamonga amewashukuru wananchi hao kwa kuweza kumpitisha bila kupingwa .
“Nimekuja hapa ndugu zangu kwanza kuwashukuru,kwa kunipa heshima hii ya kunipitisha bila kupingwa Mimi na Diwani mwezangu Erasto Mhagama lakini nimekuja kuwaomba oktoba 28 mwaka huu chonde chonde kura zote kwa Dkt John Magufuli.”amesema Kamonga
Amefafanua kuwa Rais Dkt. Magufuli amefanya mambo mengi kwenye wilaya ya Ludewa na moja wapo ni ujenzi wa barabara ya lami kiwango Cha zege unaondelea kutoka Njombe hadi Ludewa .
Pia ndani ya miaka mitano wameweza kuboresha sekta ya elimu na afya katika wilaya yao.
Kamonga ameendelea na kampeni zake katika Kijiji cha Mkiu kilichopo kata ya Lubondo ambacho nako Diwani wake amepita bila kupingwa na kuwaomba  wananchi kutofanya makosa na badala yake kura zote wahakikishe zinakwenda kwa Dkt Magufuli .
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya