Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Seoul
Zaidi ya waumini 4,000 wa Kanisa la Shincheonji Church of Jesus mjini Seoul, Korea Kusini ambao wamepona virusi vya Corona (COVID-19) watatoa utegili wao (plasma) kwa ajili ya utafiti juu ya ugonjwa huo.
Plasma ambayo ni majimaji yanayobaki kwenye damu baada ya kuondolewa kwa seli za damu inatarajiwa kutumika katika utafiti wa tiba ya Covid-19. Thamani yake inakadiriwa kufikia sh.trilioni 192.394 za kitanzania kwa kila mmoja kujitolea nusu lita.
Wamarekani wanadai kuwa, ni vigumu kupatikana kwa dawa dhidi ya corona kwa uharaka kutokana na utayari hafifu wa wagonjwa waliopona kujitolea plasma zao ambapo ni 200 tu waliokuwa na utayari wa kujitolea.
Kwa mujibu wa Afisa mmoja wa Kampuni ya Green Cross Pharma kutoka Korea Kusini, kiwango hiki kikubwa cha msaada kutoka kwa wagonjwa hao waliopona kutoka Kanisa la Shincheonji Church of Jesus italeta utatuzi wa ukosefu wa plasma kwa ajili ya utafiti.
Aidha,taarifa kutoka kanisani hapo zimeithibitishia TimesMajira Online kuwa, kati ya Februari na Machi, mwaka huu virusi hivyo viliwaathiri waumini hao ikiwa ni rekodi kubwa ya awali nje ya chimbuko la ugonjwa huo ulioanzia nchini China.
Zaidi ya watu 5,213 na visa 12,484 vilihusishwa moja kwa moja na kuenea kwa virusi hivyo kanisani, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini Korea (KCDC).
Mwanzilishi wa kanisa hilo, Man Hee Lee amesema, waumini wa kanisa hilo wameombwa kujitolea utegili kwa hiari yao wenyewe.
“Ni kama Yesu alivyojitoa sadaka kwa damu yake kwa ajili ya uhai, na tumaini letu ni kwamba utegili huu watu waliojitolea utaleta matokeo chanya katika kulishinda janga hili.
“Tulikuwa na majadiliano na maafisa wa afya ili kutengeneza mpango madhubuti kwa undani zaidi, kwa ajili ya utoaji wa msaada wa plasma, baadhi ya waumini waliopona wameshaanza kujitolea, tunashukuru kwa usaidizi wa serikali na timu za matibabu, kwani wameonesha utayari wao wa kujitolea kwa jamii,”amesema.
Awali, Jiji la Daegu nchini Korea Kusini ambalo waumini wengi wa kanisa waliathirika lilipeleka mashtaka dhidi ya kanisa kwa madai kwamba, kanisa halikutoa ushirikiano kwa wa kuowanisha idadi kamili ya waumini na vifaa vya kanisa ikiwa ni jitihada za jiji katika kukabiliana na virusi hivyo, hivyo kutaka lilipe fidia ya dola milioni 82.75.
Hata hivyo, kanisa la Shincheonji lilisisitiza kuwa, lilisema limetoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali.
“Hakuna ushahidi ulioletwa kwamba Shincheonji ilitoa orodha ambayo imebadilisha au haijakamilika na kulikuwa na utofauti mdogo tu,”amesema Kim kang-lip Naibu Waziri wa Afya, Utafiti wa Kitaalamu kwa Shincheonji.
Amesema, kuhusu Covid-19 kanisa lilitoa orodha kwa wanachama wa Korea Kusini, siku sita baada ya ombi la orodha hiyo na ilikuwa haijafafanuliwa kwamba vifaa na mali ambazo zilisimamishwa zilitakiwa ziwekwe kwenye orodha, pale ambapo serikali ilipoomba orodha ya mali zisizohamishwa.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Samia avuna makubwa Mikutano ya Uwili G20