December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watumishi wanne NEMC kufikishwa mahakamani kwa rushwa, uhujumu uchumi

Na Mwandishi Wetu

WATUMISHI wanne wa Baraza la Taifa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanatarajuia kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma rushwa na kuhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Dar es Salaan na afisa uhusiano TAKUKURU Doreen Kapwani, amesema kuwa watumishi hao walikuwa wakichunguzwa na TAKUKURU.

Aliwataja watumishi hao ni Deusdedith Josephat Katwale,Magori Wambura Matiku,Obadia Ludovick Mchupa ambao wote ni maafisa mazingira NEMC kutoka makao makuu na Lydia Laurent Ninondi ambaye ni mhasibu NEMC kutoka makao makuu.

Alisema watuhumiwa hao wanatarajia kusomewa mashtaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma rushwa na kuhujumu uchumi.