November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bodi za maji zapongezwa, zaombwa Ankara za maji ziwe halisi

Na Martha Fatael, TimesMajira Online

SERIKALI mkoani Kilimanjaro imeonya tabia ya baadhi watumishi wa Mamlaka za Maji safi na usafi wa mazingira kuacha kubambikiza wananchi ankara za maji jambo ambalo husababisha kusitishiwa huduma.

Aidha serikali imetaka watumiaji wa huduma za maji kulipa Ankara zao kwa wakati ili kukwepa usumbufu wa kusitishiwa huduma lakini pia kuziwezesha mamlaka kujiendesha.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai amesema hayo wakati anazindua wiki ya maji mkoani hapa yenye kauli mbiu maji Chini ya ardhi hazina isiyoonekana kwa maendeleo endelevu.

Amesema ni vyema kwa Mamlaka kuhakikisha wananchi wanalipia gharama za maji kulingana na matumizi yao badala ya misuguano isiyo ya lazima na wananchi.

Kagaigai alitaka bodi ya Maji bonde la Pangani (PBWB) kudhibiti ujenzi wa Makazi na shughuli za kibinadamu katika vyanzo na kingo za mito.

Katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa amesema zaidi ya wananchi
324,797 katika vijiji 179 mkoa wa Kilimanjaro, wanatarajiwa kunufaika na huduma ya majisafi katika kipindi kifupi, tangu kuwapo madarakani kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha serikali imetoa zaidi ya Sh Bil 3.5 kutokana na fedha za Covid 19 na kwamba Fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi Saba katika wilaya zote sita za mkoa huo.

Uzinduzi huo umefanywa kwa ushirikiano baina ya Mamlaka za Maji safi na usafi wa mazingira Mjini Moshi (Muwsa), Same (Samwasa), Rombo (Rombowssa) na bodi ya maji bonde la Pangani PBWB.

Amesema kwa mwaka wa fedha 2021/2022 serikali Mamlaka ya Maji na vijijini (Ruwasa) imetengewa Sh Bil 12.3 kwa ajili ya miradi 27 katika vijiji 179 mkoani hapa.

Kagaigai amesema pia Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Mjini Moshi (Muwsa), imetengewa.Sh Bil 16 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Maji kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Mkuu wa mkoa amepongeza Muwsa kwa kuboresha huduma ya Maji katika maeneo mapyanya huduma kwa kata 12 katika halmashauri ya Moshi.

Amesema thamani ya utekelezaji wa miradi hiyo ni Sh Bil 11.3 na.kwqmba hadi sasa miradi hiyo imetekelezwa kwa asilimia 31.3 kwa thamani ya Sh Bil 2.7

Hata hivyo mkuu wa mkoa ametaka Ruwasa kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati lakini pia kutosita kuwaondoa watakaoshindwa kufanya kazi kwa utaratibu uliowekwa.

Mapema mkuu wa kitengo Cha mipango na Biashara wa Muwsa, Tumaini Marandu amesema Mamlaka inepanga kutekeleza miradi mine ya kuongeza kiwwngo Cha maji na kufikia mitabza ujazo 23,067.

Amesema vyanzo vinavyoingezwa ni Chemi Chemi ya Karanga mita za ujazo 2,592, Miwaleni mita za ujazo 2,592, Mkolowonyi mita za ujazo 1,296 na Njoro ya Dhobi mitanza ujazo 16,587.

Naye mkurugenzi wa PBWB, Segule Segule amesema pamoja na kutunza vyanzo vya maji lakini wameendelea Kuweka mipaka ili kuepuka uharibifu wa mazingira.

Wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa bonde la Pangani PBWB Segule Segule akifuatiwa na mkurugenzi wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira(Muwsa) Kija Limbe na washiriki wengine kwenye uzindizi wa wiki ya maji mkoani Kilimanjaro
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai kwenye uzindizi wa wiki ya maji mkoani hapa
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya wa Moshi Abbas Kayanda