May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bashungwa asikitishwa  miradi ya afya kutokamilika

Na Esther Macha,Timesmajira Online

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Innocent Bashungwa amesema  wizara yake imetoa zaidi ya bil.243.9 kwa  ajili ya miradi ya afya 233 ambapo kati ya hiyo 110 imetekeleZwa kwa awamu ya kwanza wakati mingine iliyobakia ni kwa halmashauri  ambazo hazifanya vizuri nchini .

Bashungwa amesema hayo leo wakati alipofanya ziara  ya kukagua miundo mbinu ya majengo katika hospitali ya wilaya  Igawilo ambapo hajaridhishwa  na baadhi ya miradi kutokamilika kwa wakati  na kutoa muda wa` wiki moja iwe imekamilika .

“Wakuu wawilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini ambao watashindwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa zahanati,vituo vya afya na hospitali za wilaya ifikapo April 30 mwaka huu watawajibishgwa  na kutoa sababu kwanini wasichukuliwe hatua”amesema Bashungwa.

Aidhaameagizawakuu wa mikoa wote nchini kuwasimwa Spika wa Bunge na Mbunge wa jimbo laMbeya Dkt. Tulia Ackson kwa kujiletea maendeleao na badala yake  viongozi hao wakiwa miongoni mwa watakaochukuliwa hatua na wizara amia wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuhakikisha muda uliopangwa na wizara miradi yote inatekelezeka katika fedha za awamu ya kwanza  ya pili .

“Nitasikitishwa na viongozi wa mkoa wa mbeya ambao watashindwa kusimamia miradi ya maendeleo kushindwa kutumia fursa za uwepo  itawachukulia hatua Wakuu wa Wilaya ,Wakurugenzi wa halmashauri  watakaoshindwa kukamilisha miradi ya afya ifikapo April 30 mwaka huu na kuagiza wakuu wa Mikoa nchini  kuwasimamia”Amesema Waziri Bashungwa..

Hata hivyo Waziri Bashungwa amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Triphonia Kisiga kuhakikisha miradi hiyo inakwenda kwa kasi ili Mbeya ipige hatua kwani kwa sasa kama Wizara watahakikisha linakuwa la kisasa zaidi .

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa ,Juma Homera Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ,Dkt. Rashid Chua chua amesema kuwa kwa maslai mapana ya Taifa watasimamia kuona miradi yote inakamilika kwa wakati.

Dkt. Chua Chua amesema kuwa ifikapo April mwaka huu 30,mwaka huu miradi yote ya ujenzi na ukarabati ya miundombinu katika hosptali za Wilaya, Vituo vya afya na Zahanati vinakamilika kwa wakati.

Amesema kuwa miradi yote iliyobaki itakamilika kwa wakati kama walivyopanga.