Na Penina Malundo,TimesMajira,Online
KAMISHNA Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Mkadam Khami amesema katika kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka huu jumla ya shule 5,320 na wanafunzi 592,396 wamepatiwa elimu juu ya usalama barabarani huku vijiwe vya bodaboda 11,760, madereva wa bodaboda 212,464 wamepatiwa elimu hiyo.
Pia takribani stendi za Mabasi 3,589 zilifikiwa katika utoaji wa elimu hiyo, mabasi yakiwa 1,182,366 na i abiria 6,874,225 walipata elimu ya usalama barabarani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Mkadam Khami wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha yao kutokana na Ajali za Barabarani,ikienda sambamba na utoaji wa vyeti kwa wachora katuni waliotoa mchango wao katika uchoraji wa katuni kuelimisha jamii.
Amesema jeshi hilo limekuwa likikazia usimamizi wa Sheria ya usalama barabarani kwa kufanya operesheni mbalimbali za usalama barabarani na kuhakikisha linatoa elimu ipasavyo kwa watumiaji wa barabara.
ACP,Khami amesema wamekuwa wakijitahidi kuthibiti makosa hatarishi kama vile mwendo kasi, kupima ulevi, kusimamia madereva kufuata michoro ya barabarani.
“Tumekuwa tukiitumia mihadhara mbalimbali kama maadhimisho ya nikita nenda kwa usalama barabarani katika maonyesho kama ya saba saba na ya nane nane kutoa elimu,”amesema na kuongeza
“Teknolojiaya habari na Mawasiliano imekuwa ya msaada mkubwa katika kuhakikisha kwamba madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani wanadhibitiwa,”amesema
Aidha amesema katika kukazia usimamizi wa sheria wamekuwa wakifanya operesheni mbalimbali za uslama barabarani kudhibiti makosa hatarishi yakiwemo mwendokasi,kupima ulevi,kusimamia madereva kufata michoro ya barabarani.
Mkurugenzi wa Mpito wa Tanzania Media Foundation,(TMF),Fausta Musokwa amesema uandishi wa habari wenye maslahi kwa umma unaweza kusaidia kuimarisha usalama barabarani.
“TMF ni taasisi inayofanya kazi kuimarisha uandishi wa habari wenye maslahi kwa umma na kushirikiana na wadau mbalimbali ili kujenga uwezo katika sekta ya habari Tanzania, “amesema
Amesema habari za usalama barabarani zimechangia kuboresha usalama barabarani na kumgusa kila mmoja imemgusa na kubadilishana mtazamo wa watu na kupaza sauti lengo likiwa kuokoa maisha yao.
“Leo siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha yao kutokana na ajali za barabarani ni vema kutambua usalama barabarani ni vyema waandishi wa habari kuzingatia sheria na misingi ya uandishi kwa kushirikiana na Polisi ili kupata taarifa sahihi na kutoa haki ya kujibu,”amesema
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya