December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watumiaji barabara watakiwa kufuata sheria

Na Zuhura Mohamed, TimesMajira Online

Dawati la usalama barabarani limetoa wito kwa kundi la watumiaji wa barabara kwa njia ya miguu wakiwemo wasukuma mikokoteni kuzijua na kuzifuata sheria Pamoja na alama za barabarani ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

Akizungumza na Gazeti la Majira Sajent Amin {jana Oktoba 19 2022} alisema kufuata sheria hizo ni haki ya kila mmoja kwa usalama wake Pamoja na watumiaji wengine wa barabara.

Aidha Sajent Amin aliesema kuwa kundi hili ni kundi ambalo upatikanaji wake ni mgumu kutokana na shughuli wanazofanya pia alisema ni kundi ambalo linahisi kuwa wao hawana ulazima wa kuzijua sheria na alama za barabarani kwasababu wao ni watembea kwa miguu kitu ambacho sio kweli.

‘’Kundi la watembea kwa miguu, waendesha mikokoteni ni kundi ambalo ni vigumu kulifikia kwa urahisi kutokana na shughuli zao za kiuchumi pia kundi hilo ni kundi ambalo huwa wanahisi hakuna umuhimu wao kuzijua au kupata elimu kuhusiana na usalama pamoja na sheria za barabarani’’.Alisema Sajenti Amin

Pia alisema kuwa kutokujua sheria siyosababu ya kuvunja sheria hivyo ni muhimu kujifunza na kupata elimu kuhusiana na sheria za barabarani kwasababu kutokujua sheria sio kigezo cha kutofuata sheria husika.

Hata hivyo Godfrey Hamza mkazi wa Posta alisema kuwa watu wengi hawana elimu kuhusiana na usalama barabarani kwasababu huwa hawana muda wa kufuatilia maswala hayo ambayo ndio msingi mmoja wapo wa kulinda Maisha yao.

Pia alisema kuwa ili watumiaji wa barabara waweze kujifunza na kuona umuhimu wa kufuata sheria ni muhimu kutafuta njia za kuwafikia kwa wakati waenda kwa miguu hata ikiwezekana watumie njia za burudani ili kufikisha elimu.

‘’Ili watumiaji wa barabra waweze kujifunza na kufuata sheria ni m8uhimu kutafuta njia za kuwafikia kwa wakati na kuwapa elimu waenda kwa miguu ikiwezekana watumie njia za burudani ili kufikishga elimu kwa wtu husika’’. Amesema Godfrey