April 23, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watiani 84 warejesha fomu za ubunge majimbo manne Wilaya ya Ilala

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online -Ilala

Watiania wa nafasi ya Ubunge 84,ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), kutoka majimbo manne ya Wilaya ya Ilala ambayo ni Ilala,Segerea,Ujinga na Kivule,wamefanikiwa kurejesha fomu za kuwania nafasi hiyo ndani ya chama.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar-es- Salaam,Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Silivester Yared,amesema mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu dirisha lilifungwa Julai 2,2025, saa kumi kamili.Ambapo katika zioezi hilo watiania 87 waliochukua fomu huku walifanikiwa kurejesha ni 84 .

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Chanika Wiliam Mwila (kulia) akirejesha fomu ya Ubunge kugombea Jimbo la Ukonga kwa Katibu wa Wilaya ya Ilala Sylvester Yaredi

Amesema,katika Jimbo la Kivule waliochukua fomu ni 46 huku waliorejesha ni 44,Jimbo la Segerea walichukua 18 waliorejesha ni 17,Jimbo la Ukonga walichukua 11 na wamerejesha 11 huku Jimbo la Ilala walichukua 12 na wamerejesha 12.

Mmoja wa watia nia nafasi ya Ubunge Jimbo la Kivule,ambaye amefanikiwa kuchukua na kurejesha fomu ni Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Vijana CCM,wilayani Ilala,Wakili Alfred Tukiko Oktchi.

Wakili Tukiko amesema,anazijua chagamoto zinazowakumba wakazi wakivule na kusisitiza kuwa yeye ni mtu sahihi kwa maendeleo ya wanakivule .

“Nimekuwa kiongozi wa nafasi mbalimbali,nimejipima na kuona natosha kuwaogoza wananchi wa Kivule ili ni Jimbo Jipya niweze kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo,”.

Kada wa CCM Wilaya ya Ilala Tickey Kitundu (kulia)akirejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Jimbo la Kivule kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Sylvester Yeredi

Wengine waliorejesha fomu za Ubunge,ni Anita Waitara,Mzee Yusuph wa Jahazi Taarabu,Diwani Mstaafu Aidan Kwezi,Bonah Ladslaus Kamoli,Jerry Silaa,Ojambi Masaburi,Askari Joseph Malangu,Diwani Tickey Kitundu,Mhandisi Amiri Abdalah Muhando,Masunga Masele,Angelina Akilimali kutoka Radio Uhuru,Frederick Lwegasira,Chacha Wambura Nchama,Rais wa Filamu Tanzania Rajabu Amiri,Mwinyijuma Seke Ragi Samwel.

Wakili na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Ilala Alfred Tukiko(kulia) akirejesha fomu ya kuomba ridhaa ya nafasi ya Ibunge Jimbo la Ukonga kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Srilvester Yared