November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watengenezaji wa vimiminika visivyo na kilevi watoa ombi kwa serikali

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Watengenezaji wa vimiminika visivyokuwa na kilevi vinavyotokana na matunda Kama vile Mocktails, Smoothie, Tendeshake na Milkshake, wajulikanao kama Nica Juice bar, wameiomba serikali kuwaangalia zaidi vijana ambao wameanzisha biashara zao ndogondogo hasa kwa kuwapa tenda kwenye mikutano ya serikali ili kuwawezesha biashara zao kukua zaidi.

Akizungumza na TimesMajira Tv, Mkurugenzi wa Nica Group Enterprises, Veronica Hekwe amesema mbali na serikali lakini pia wadau mbalimbali wakiwemo wateja waweze kushirikiana kwa pamoja kwa kuwaunga mkono na Kuwapa kazi.

Mkurugenzi huyo amesema Kitu Kikubwa ambacho kinawatofautisha na wafanyabiashara wengine ni kunamjali mteja kwa wale wanaofika ofisini lakini pia wanaowapelekea bidhaa yeo sehemu mbalimbali, wanamuhudumia mjeta aridhike, wanamlinda mteja kwa kuhakikisha vimiminika vyao vinakua katika mazingira safi na salama

Aidha Mkurugenzi huyo amesema katika majukwaa ambayo wanahudhuria huwa wananufaika Sana kwa kukutana na watu mbalimbali kuwapa elimu ya Afya na kufahamiana zaidi;

“Majukwaa yanatunufaisha sana kwasababu tunakutana na watu wengi na kuwapa elimu kubwa ili waweze kuhamia kwenye kutumia vimiminika ambavvyo ni asilia lakini pia tunafaidika kwa kuikuza biashara kupitia watu tunaokutana nao wanakua wanatutambua kwa haraka na kuweza kubadilishana mawasiliano kwa urahisi”

Pia Hekwe amesema Mwaka 2020 waliandaa mafunzo kwa watu Mbalimbali ili kuweza kujua namna ya kufanya biashara hiyo ya juice na wapo ambao hadi sasa wameshaanza biashara zao za kuuza juice kupitia elimu waliyoitoa

Mkurugenzi huyo amesema mbali na kuandaa mafunzo kwa watu mbalimbali lakini pia kwa miaka miwili ijayo wanampango wa kufungua chuo kikubwa kwaajili ya mafunzo ya biashara hiyo ya Juice ili kutoa elimu zaidi watu wapate mafunzo na kupata uelewa kuhusu biashara hiyo;

“Malengo yangu baada ya miaka miwili nitaanzisha chuo kwaajili ya kuweza kuwafundisha watu zaidi na nahitaji kugusa zaidi vijana ili kuweza kuwasaidia waweze kuinuka kujitegemea kuachana na dhana ya kwamba biashara ya matunda siyo biashara inayofaa”

Nica Juice bar inapatikana Makumbusho kijitonyama, na Kila mwisho wa mwezi hutoa zawadi kwa wateja ikiwemo punguzo la bei ya juice na zawadi kama karanga, ndizi n.k