Na Penina Malundo,timesmajira,Online
WAZIRI wa nishati, January Makamba amewataka watanzania kutoweka vikwazo katika kutafuta njia pekee ya kuondokana na nishati chafu badala yake watafute njia Mbadala na kuchangia mawazo ya nini kifanyike ili kurahisisha upatikanaji wa nishati safi na salama ya kupikia kwa Taifa zima .
Aidha amesema kuwa ili kupata mafanikio kwa taifa zima ya upatikanaji wa Nishati safi na Salama serikali itahakikisha Sera ,sheria na mifumo madhubuti inawekwa vizuri huku akiwataka wadau ambao wanafikiri kuanzisha nishati safi mbadala kujitokeza kwani atashirikiana nao katika kutatua changamoto hiyo.
Nae Mbunge wa jimbo la Manonga na Makamu Mwenyekiti Kamati ya kudumu ya Nishati na madini Seif Khamis Gulamali akishiriki mjadala huo amesema ni kilio cha muda mrefu cha Kamati na wabunge kwa ujumla na wananchi juu ya matumizi mbadala ya Nishati.
“Ni kilio cha muda mrefu cha Kamati na wabunge Kwa ujumla na wananchi juu ya matumizi mbadala ya Nishati ya mkaa na kuni Kwa sababu tumeona madhara ambayo yanatokea katika jamii zetu.
Aidha,amesema kukatwa kwa misitu si tu inaharibu mazingira na bali pia inaathiri upatikanaji wa mvua.
“Mnapokata Miti maana yake kunakuwepo Kwa janga la ukosefu wa mvua na njaa ambayo inawaumiza wananchi wenyewe wananchi” Seif Khamis Gulamali, Mbunge wa jimbo la Manonga na Makamu Mwenyekiti Kamati ya kudumu ya Nishati na Madini.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja