January 7, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watanzania washauriwa kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini

Na David John, TimesMajira Online, Pwani

MKURUGENZI wa Kampuni ya Mtanga PolyMachinery Heri Mtanga amewataka Watanzania kuwa wazalendo na kupenda kutumia bidhaa ambazo zinatengenezwa nchini ili kusaidia kuchochea maendeleo.

Amesema kuwa kumekuwepo na kasumba ya watanzania kupenda vitu vya kigeni kuliko vya nyumbani hivyo niwakati mwafaka sasa kuona Umuhimu wa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na makampuni ya ndani.

Heri Aloyce Mtanga ameyasema haya wakati Akizungumza na TimesMajira online hivi karibuni kuhusu uzalendo wa kutumia vitu vinavyozalishwa nchini ili kuendelea kuimairisha uchumi wa Tanzania.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mtanga PolyMachinery ya Mkoani Pwani Kibaha picha ya ndege Heri Aloyce Mtanga akionyesha aina mbalimbali za machine anazotengeneza kwenye karakana yake.ambapo pia machine hizo zilikuwa sehemu ya maonyesho ya sabasaba.

Mtanga ambaye anamiliki karakana ya kutengeneza mashine ambazo zinatumika kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwamo machine za kutengeneza sababuni,mafuta ya kupakaa, machine za kuchakata mafuta, machine za kutotolesha vifaranga,pamoja na matofari.

“Ndugu Mwandishi kuna tatizo kubwa sana la uzalendo Kwa maana watu kupenda bidhaa zinazozalishwa nchini lakini pia kuunga mkono jitihada zinazofanywa na vijana wakitanzania za kutoa ajira Kwa watanzania wezao” Amesema Mtanga

Akizungamzia safari yake hadi kumiliki kampuni na karakana ya ufundi,amesema kuwa awali alikuwa Mwalimu wa Sayansi ambapo alikuwa anafundisha moja ya Shule ya sekondari Wilayani Bagamoyo na baadae kujiunga Chuo Kikuu  lakini hakufanikiwa kumaliza kutokana na changamoto ndipo akaamua kufungua karakana ya ufundi.”

Amesema kuwa hivi sasa anatengeneza mashine aina mbalimbali zaidi ya 20 na ametoa ajira Kwa vijana zaidi ya 25 kwenye upande wa ufundi lakini kwenye uzalishaji wa bidhaa kuna watanzania wengi ambao wanaendesha maisha yao kupitia bidhaa zinazozalishwa na Mtanga PolyMachinery Kampuni inayopatikana Kibaha Picha ya ndege.

Mkurugenzi Mtanga pia ametoa ushauri Kwa taasisi za Serikali na viongozi waliopewa mamlaka kujenga nidhamu na tabia ya kuwaunga mkono vijana wakitanzania ambao wanathubutu kuleta Mapinduzi ya kiuchumi.

Amesema kuwa  vijana wanapambana katika kuhakikisha wanachangia kukuza uchumi wa nchi yao lakini pamekuwepo na ufinyu wa kuungwa mkono hasa kupitia taasisi za Serikali ambazo ndizo zenye nafasi kubwa ya kufanya hivyo.

Mkurugenzi Mtanga ambaye historia yake ni Mwalimu ambaye aliamua kuacha kazi hiyo na kujikita katika kujiajiri na kuazisha Kampuni ambayo kwasasa inadhalisha vijana wengi wa kitanzania kwenye eneo la ufundi.

“Hapa nataka kusema leo hii Mtanga imetoa fursa za ajira Kwa vijana wengi tu Kwa mfano katika karakana yangu ninavijana mafundi zaidi ya 20 lakini nje ya karakana nina kundi kubwa la watanzania ambao leo hii wanaendesha maisha yao kupitia bidhaa zinazozalishwa na Mtanga PolyMachinery  kampuni.” amesema

Kuhusu vijana wasomi.

Mtanga Amewataka vijana kuacha kutegemea ajira za Serikali badala yake wachangamkie fursa mbalimbali ambazo zinajitokeza ikiwamo sekta ya ufundi ambayo Kwa asilimia kubwa inamwandaa kijana kujitegemea.

Mkurugenzi huyo ambaye mawasiliano yake ni 0789 988597 amesema kuwa kupitia karakana yake amewaalika vijana kwenda kupata elimu ya ufundi ambapo hapo atapata ujuzi wa kutengeneza machine za aina mbalimbali zikiwemo za kutengeneza sabuni, mafuta pamoja na zinginezo.