November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watanzania kunufaika na Taxi Mtandao

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

ZAIDI ya Watanzania elfu kumi hadi laki moja wanatarajia kunufaika na ajira na kuondolewa changamoto ya usafiri baada kuzundiliwa kwa Application ya Taxi mtandao ijulikanayo Kama Swiftcabb inayomilikiwa na Tanswift Company limited ikiwa lengo ya kuunga mkono jitihada za serikali kuiwainua vijana.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Transwipt,Japheta Tesha,wakati wa uzinduzi ufunguzi wa huduma hiyo.

Aidha,Tesha amesema huduma hiyo itawasaidia madereva Bodaboda kutumia kupata Abiria na pia kuwasaidia Abiria kupata usafiri kwa haraka .

“Tumeamua kutoa Ajira kwa vijana na tunatarajia kutoa ajira elfu kumi za moja kwa moja na ajira mia tano rasmi,tukiwa na lengo la kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassani za kukuza uchumi”Amesema Tesha.

Hata hivyo ,Tesha amebainisha kuwa huduma hiyo ya Taxmtandao imeanza Dar es Salaam inatarajia kwenda mikoa ya Arusha na mwanza.

“Huduma yetu tunakata asilimia 15 kwa dereva, kwa sasa tunawatumia wanafunzi wa vyuo vikuu kufanya kazi ya masoko,wanafunzi wataweza kupata kipato kupitia kazi ya masoko”Amesema Tesha.

Kwa upande wake,Frola Mgonja,kutoka ofisi mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa anamwakilisha mgeni mkuu wa Mkoa wa hapa,Amosi Makalla,amewata madereva wa Bodaboda kwenda ni wakati na kuanza kutumia za kidigitali.

“Dunia imebadilika mambo yote kidigitali,nawaomba Bodaboda kuacha kusubilia Abiria kijiweni badala yake watumia mtandao wa Swiftcabb kujipatia Abiria kwa haraka”Amesema Mgonja,

Mgonja ameipongeza kampuni ya Tanswift Company limited kuja na huduma hiyo na kusema itasaidia kukuza kipato kwa vijana na kuendana na maono ya Rais Samia ya kuleta maendeleo nchini.

Mwenyekiti wa Chama chaj bodaboda mkoa wa Dar es Salaam, Maichael Masawe,amesema huduma ya Swiftcabb kwao itakuwa mkombozi kwa Bodaboda itaweza kuwaongezea kipato,