Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online- Mwanza
KUTOKANA na malalamiko yaliotolewa na baadhi ya wananchi wa Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela mkoani Mwanza,wakidai kuwepo kwa watoto wanayofanya vitendo vya uhalifu katika maneno yao, viongozi wa Serikali za Mitaa wametakiwa kutimiza wajibu wao.

Wananchi hao walitoa malalamiko hayo Juni 28,2026 mbele ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP.Wilbrod Mutafungwa, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Kona ya Bwiru, Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela mkoani humo na kuhudhiriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ilemela Kafiti Kafiti.
Awali mmoja wa wananchi wa mtaa wa Nyamanoro Mashariki Niael Said,amelalamikia kero ya uwepo wa watoto wanaojihusisha na uhalifu mitaani, hasa eneo la Kona ya Bwiru na daraja la watembea kwa miguu la Furahisha, kuwa wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya uhalifu.
“Kamatakamata imezidi,sasa hivi tukiwaona Polisi tunakimbia lakini mtulegezee, mnafanya kazi nzuri,”amesema Ally Abdallah, dereva wa bodaboda.
Akizungumza na wananchi hao baada ya kusikia kero na ushauri kutoka kwao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP.Wilbord Mutafungwa amewatoa hofu wananchi huku akitoa wito kwa viongozi wa Serikali za Mitaa,Watendaji wa Vijiji na Vitongoji kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ya kazi.Pia kuwaondolea hofu ya usalama wananchi ili waendelee kufanya shughuli zao za kila siku na kujiletea maendeleo.
DCP.Mutafungwa amesisitiza kuwa kamatakamata ya wahalifu itaendelea kulingana na namna ambavyo wahalifu watapungua katika maeneo yao.kwani awali wananchi walieleza kukerwa na uwepo wa wahalifu eneo la Kona ya Bwiru na Daraja la watembea kwa miguu la Furahisha.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Kafiti Kafiti,ameshauri mikutano kama hiyo iwe endelevu katika maeneo mengine ndani ya Mkoa wa Mwanza.
Huku akiwahimiza wananchi kuilinda amani ya nchi na kwani jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi huku akiwasisitiza kuthamini mchango unaofanywa na askari wa Jeshi la Polisi katika kulinda raia na mali zao.
“Kuna wakati unaweza kuona kama Polisi hawafanyi kazi, lakini nawaambia wakienda likizo mwezi mmoja tu mtaona umuhimu wa hawa watu,”amesema Kafiti.



More Stories
Rais Samia kufungua Mkutano wa TMIC 2026
Watakiwa kumtetea Rais kwa hoja si hisia
Yas Business,FTCC wawajengea uwezo Wajasiriamali