May 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watakiwa kupuuza taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii

Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbarali

MBUNGE wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya Francis Mtega amewataka wananchi kupuuza taarifa zinazopotoshwa na baadhi ya wanasiasa mitandaoni wenye nia ovu na Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mtega amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Chimala Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuzindua soko la wafanyabishara sambamba na stendi ya mabasi Iliwa,mradi wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya.

Mbunge wa Jimbo la Mbarali Francis Mtega akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM baada ya kukata utepe akiashiria kuzindua soko la wafanyabiashara kata ya Chimala.

“Mitandao ya kijamii ina nia kukichafua Chama kilichopo madarakani kwamba wabunge waliopo bungeni wameshindwa kuisimamia serikali kufuatia taarifa iliyotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) jambo ambalo sio sahihi ni kupotosha umma”amesema.

Mtega ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya hesabu za Serikali ,amesema yeye ndiye mwakilishi wa wananchi wa ana fahamu ukweli na ndo mtu sahihi anayeweza kutoataarifa hivyo amewataka wananchi kuwa na imani na Serikali fedha zao ziko mikono salama.

‘’Wakati taarifa hiyo imekwenda kukabidhiwa kwa Rais,kulikuwa na suala lingine la ununuzi wa ndege ya mizigo ilibakia fedha kidogo ambayo tayari serikali imeshalipa bil.37 akashangaa kuona hati ya madai inayodai bil.80….,bahati nzuri tayari serikalitayari inalifanyia kazi inachunguza wapo wanaowekwa pembeni lakiniwengine ufuatiliaji unaendelea kufanyika’’amesema Mbunge Mtega.

Mbunge wa Jimbo la Mbarali Francis Mtega akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua soko la wafanyabiashara Kata ya Chimala.

Mtega amewataka wananchi wasikubali kubabaishwa na watu wachache wanaoichafua serikali na kubainisha kuwa wakati wa siasa bado haujafika na badala yake waipishe ili iendelee kuboresha huduma muhimu kwa wananchi ikiwemo elimu,afya,miundombinu ya maji na barabara.

“Ndugu zangu nimefanya mambo makubwa ya kuishawishi Serikali ikiwemo kutatua changamoto ya mgogoro wa mashamba, kumuomba Rais mradi wa ujenzi wa mabwawa ya kilimo cha umwagiliaji ambao tayari tunajengewa skimu sita ambazo zitaboresha kilimo cha mpunga ”amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Chimala,Wille Blankison amesema kuwa historia inaonesha kuwa kata hiyo haina soko na kwamba masoko mengi yapo kwenye vilabu vya pombe ndio yanaitwa masoko.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chimala Wille Blankison,akizungumza na wananchi mara baada ya uzinduzi huo.

Huku akisema kuwa historia ya Chimala hakuna sehemu rasmi ya stendi ya magari hivyo Jumuiya ya Wazazi CCM ikaona ni vema kutoa eneo kwa ajili ya soko na kuegesha magari .

Amesema kuwa Kata ya Chimala imekuwa na changamoto ya masuala ya siasa na kusahau kuwa siasa ina wakati wake kuna wakati wa kuzungumzia siasa na maendeleo wakati wa siasa ukifika watasema.

‘’Sasa nawashangaa wana Chimala eti mimi siwezi kuwekeza eneo hilokwakuwa ni la CCM nawaomba wana Chimala ifike wakati mbadilike nduguzangu tunabadiishe Chimala yetu kwa kushirikiana , wewe ukichukuakibanda hapa inakuwa manufaa kwako wewe na familia yako ‘’amesemaMwenyekiti huyo .

Mjumbe Kamati ya Utekelezaji Wilaya ya Mbarali Sebastian Kibiki,amesema ni wakati kwa wanaCCM kushirikiana na kukisemea chama vizuri ili kuwatia moyo viongozi wanaofanya kazi za wananchi hususani Mbunge wa Jimbo la Mbarali Francis Mtega.

Mfanyabishara wa miwa Sijali Musa amesema katika uchaguzi Mkuu 2025 watajitoa kwa mvua na jua kuhakikisha Mbunge wao anarejea katika nafasi yake kwani wanaona namna anavyo wasilisha kero kwenye vikao vya bunge zinazowakabili ikiwe kwenye sekta ya Kilimo.