Na Mwandishi wetu,Majiratimes,Online
WITO umetolewa kwa Wastaafu nchini kuhakikisha wanatumia taasisi za kifedha kuzitumia ili kupata usalama, tija ya mafao yao na kuepukana na vishoka wa mtaani.
Wakizungumza hayo leo mkoani Mtwara,wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa wastaafu watarajiwa yaliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF),wamesema taasisi hizo zimesema wastaafu hupata pesa nyingi kwa wakati mmoja ni vyema kuzihifadhi benki ambako watapata faida ya riba, mikopo na elimu ya kifedha.
Meneja Mwandamizi Miamala na Maendeleo ya Biashara kutoka Benki ya Walimu, Yebete Zablon amesema wastaafu watarajiwa wanapaswa kutumia fursa za zilizopo katika taasisi za kifedha na sio kuishia kwa vishoka ambapo wamekuwa wakiwaumiza kwa riba kubwa.
“Badala ya kukopa kwa riba kubwa kutoka kwa vishoka wa mtaani,mnayo fursa ya
kukopa kupitia mkopo wa “mlinde mstaafu’ ambapo wastaafu wa umma wakiwemo walimu wanaweza kulipwa pesa ya mshahara kiasi kile kile walichokuwa wanapata kila mwezi,”amesema na kuongeza
“Wastaafu watarajiwa wenye mishahara mikubwa sana watalipwa asilimia 15 ya pesa kila mwezi au kuomba kiasi kikubwa lakini kisivuke sh Milioni 10,”amesema
Naye Mwakilishi wa Benki ya Taifa ya biashara,(NBC) Halima Semhunge amesema benki yao ambayo ina matawi zaidi ya 80, mawakala zaidi ya 200 na mashine za kutolea pesa zaidi ya 47 na za umoja zaidi ya 260 inatoa fursa ya elimu ya kifedha kwa wastaafu kupitia dawati lao la wastaafu.
Meneja wa Benki ya Biashara ua Tanzania Commercial Bank (TCB )Mkoa wa Mtwara, Godfrey Banza amesema kuwa katika mabadiliko yaliyofanywa na serikali ya kuunganisha zilizokua benki ya wanawake, twiga, TIB na ya posta kisha kupatikana TPB inao mtaji wa kutosha hivyo kuweza kuhudumia wateja wengi wakiwemo wastaafu watarajiwa.
Meneja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mkoa wa Mtwara Emmanuel Mseti amesema wanayo akaunti ya ‘NBC shambani’ ambayo haina makato yoyote kwa ajili ya kuendeleza kilimo.
Amesema wastaafu wanaopendelea shughuli za ujasiriamali wanaweza kunufaika kwa akaunti ya ‘NBC kuwa nasi’ anbayo pia haina makato ya mwezi pia kutoa fursa ya mkopo hadi wa Milioni 50.
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti