January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Washindi wa ‘Wakishua twenzetu Qatar na Hisense’ wiki ya pili, tatu wapatikana

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni inayoongoza Tanzania katika kuhakikisha mtanzia anaishi maisha ya kidijitali Tigo Tanzania, kupitia Promosheni yake ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense kwa kushirikiana na kampuni ya HISENSE wametoa tiketi 19 za kwenda Qatar kushuhudia kombe la Dunia ( kwa washindi wa wiki ya pili ) na zawadi ya Vyombo vya ndani kama vile Friji , Spika za Mziki (SubWoofer), Smart Tv , pamoja na Microwave ambavyo vinakamilisha idadi ya washindi wa vifaa vya nyumbani za Hisense 6 na washindi wa Tiketi 21 ambazo kufikia leo zimekwishatolewa tangu promosheni hii ianze .


Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta amesema kuwa
” Hawa washindi wa leo wamepatikana kwenye Droo yetu ya wiki ya Pili na tatu ya promosheni yetu , washindi hawa walifanya miamala kama kulipa bili , kufanya malipo ya kiserikali , kupokea pesa kutoka nchi za nje , benki , mitandao mingine , LIPA KWA SIMU , kununua muda wa maongezi na huduma nyingine mbalimbali za Tigo Pesa ambapo baada ya kufanya ivyo waliingia kwenye droo na mwisho wa siku kuibuka washindi wa Kampeni hii Ya WAKISHUA TWENZETU QATAR NA HISENSE , Tunawasihi wateja wetu endeleeni kufanya miamala na Tigo Pesa ili kuibuka mshindi maana hadi kufikia leo tumeshatoa tiketi kwa washindi 21 na washindi 6 wa vifaa vya nyumbani kutoka Hisense”

” Tumebaki na tiketi 29 za kwenda QATAR kushuhudia kombe la dunia , na bidhaa 24 za vifaa vya ndani kutoka Hisense , kwahyo nawasihi mfanye miamala mingi na kutumia huduma za Tigo Pesa ili kuibuka mshindi wa zawadi hizi zilizobaki ” Alimalizia.

Naye kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya HISENSE Bwn. Joseph Mavura amesema kuwa kampuni ya Hisense inatoa ofa ya punguzo la 20% katika maduka yao yote kwa mteja atakayenunua bidhaaa na Kulipia kwa Tigo Pesa ” Alimalizia

Baadhi ya Washindi wa wiki ya tatu na ya pili , promosheni hii ya WAKISHUA TWENZETU QATAR NA Hisense ni ni Elvis Brian Otieno , Mkazi wa Kinondoni Dar Es Salaam , Fatma Said Kimaro Mkazi wa Mbezi Beach Dar Es Salaam , Kalaghe Safiel Rashid mkazi wa Tegeta , Boniface Roman Mahan Mkazi wa Dar Es Salaam , Walter Manyiri Mkazi wa Dar Es Salaam , Narcis John Mkazi wa Dodoma, na wengineo.