May 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Washauriwa kula chips wakati huu kuepuka hasara wakati huu

Na Mwandishi Wetu

BRUSSELS, Wabeligiji wameombwa kula chipsi kwa wiki mara mbili baada ya virusi vya corona kusababisha ongezeko kubwa la viazi katika maghala.

Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Viazi na wenye Viwanda nchini Ubeligiji (Belgapom), Romain Cools amesema zaidi ya tani 750,00 za viazi zipo hatarini kutupwa kutokana na kukosa watumiaji.

Cools amesema hayo katika mahojiano na Shirika la Habari la CNBC ambapo amebainisha kuwa, wazalishaji wa viazi wanakabiliwa na mgogoro mbaya ambao hawajawahi kuhushudia nchini humo.

Hayo yanajiri ikiwa Ubeligiji ilitangaza zuio la kukaa ndani kwa watu wote tangu Machi 18, mwaka huu na wanatarajia kulegeza au kuendelea hivyo mwezi ujao.

“Virusi vya corona vimesababisha wingi wa viazi ambavyo havina matumizi, tangu Serikali iweke zuio la kila mmoja kukaa ndani, hivyo biashara ya chipsi kule kwenye baa na migahawa hamna, jambo ambalo linahatarisha uchumi wetu,”anasema Cools.

Romain Cools anasema, tani zaidi ya 750,000 za viazi ambazo zitaweza kujaza zaidi ya malori 30,000 hazijulikani zitafanyiwa nini kwa sababu hakuna kinachoendelea tangu janga hilo litangazwe.

Times Majira Online umebaini kuwa, Ubeligiji ni miongoni mwa wauzaji wakubwa wa bidhaa zitokanazo na viazi duniani zikiwemo chipsi zilizokaushwa. Kwa mwaka huwa inasambaza zaidi ya tani milioni 1.5 za bidhaa hizo katika mataifa zaidi ya 100 duniani.