Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
OFISI ya Taifa ya Takwimu imesema,tangu ilipotangazaza nafasi za kazi za muda za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 hadi kufikia Mei 16 mwaka huu jumla ya watu wapatao 532,347 ,wameshaomba nafasi hizo .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa kuhusu mwenendo wa wa uombaji wa nafasi hizo , Kaimu Mkurungezi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ruth Minja amesema,mwenendo wa uombaji unaendelea kwa kasi kubwa ikilinganishwa na wiki ya kwanza tangazo lilipotolewa.
“Hadi kufikia leo Mei 16,2022 saa saba kamili mchana jumla ya maombi 532,347 kati ya nafasi 205.000 zilizohitajika ikilinganishwa na maombi 119,468 yaliyokuwa yamepokelewa na kutangazwa kwa umma Mei 9 mwaka huu .”alisema Minja
Aidha amesema,kati ya maombi hayo yaliyopkelewa,waombaji 193,548 sawa na asilimia 36 ni waajiriwa kutoka katika sekta ya umma ,sekta binafsi waombaji 58,566 sawa na asilimia 11 wamejiajiri wenyewe na waombaji 280,233 sawa na asilimia ni wale ambao hawana ajira.
Minja ameendelea kutoa wito kwa wanaotuma maombi ya ukarani au usimamizi wa maudhui au usimamizi wa tehama wafuate kwa ukamilifu maelekezo yaliyowekwa kwenye tangazo la kazi ,wajaze fomu ya maombi kwa ukamilifu na waambatanishe nyaraka zote muhimu zinazohitajika.
Vile vile Minja amewasisitiza waombaji wote kuhakikisha wanajaza namba za simu na barua pepe ambayo inatumika kwa sasa ili aweze kupokea taarifa za akaunti yake ya kuingia kwenye mfumo ili kukamilisha kutuma maombi hayo.
More Stories
Tanzania,Uturuki kushirikiana kuinua sekta ya utalii nchini
Wanaoficha watoto wenye ulemavu kusakwa
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu