May 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake watakiwa kuacha mikopo ya Kausha damu

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya UWT Wilaya ya Ilala Salma Fumbwe ,amewataka Wanawake wa Wilaya ya kuachana na mikopo chechefu inayodaiwa kausha damu badala yake wakope mikopo ya Serikali na kuchangamkia fursa za kiuchumi .

Salma Fumbwe alisema hayo katika semina ya Wanawake na vijana wa Kata ya Mzinga iliyoandaliwà na Diwani Job Isack, na Diwani wa Viti Maalum Wanawake Ilala Mwalimu Beatrice Edward .

“Wanawake wezangu na vijana wa Mzinga nawaomba mchangamkie fursa mbalimbali za kiuchumi na mikopo ya Serikali na Taasisi za Benki ambayo ya inatolewa kwa riba nafuu tuachane na mikopo chechefu inayodaiwa ya kausha damu ” alisema Salma.

Mjumbe wa Kamati ya Siasa Salma alisema kina mama wengi wanashindwa kuwajibika na Malezi ya familia zao kutokana na mikopo chechefu amewataka Wanawake kubadilika na kuchangamkia fursa za uchumi .

Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala alisema jumla ya washiriki 600 Wanawake na vijana wamepatiwa mafunzo hayo kwa vitendo Ili wajikwamue kiuchumi .

Mwl,Beatrice aliwataka wanawake na vijana waliopata mafunzo hayo kuyatumia vizuri Ili wajikwamue kiuchumi waache kuwa tegemezi.Katika mafunzo hayo walishirikiana na Wadau Benki ya CRDB ambapo washiriki waliopata fursa ya kufungua akaunti .